Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Mbarak Alhaj Batenga akisisitiza jambo wakati wa semina ya EWURA kwa wadau kuhusu kutambua na kushiriki fursa zinazotokana na bomba la Mafuta ghafi la EACOP, leo Juni 6,2023 wilayani Kiteto.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) , Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lovii Long’idu, akitoa elimu kwa wafanyabiashara, mafundi watoa huduma na wananchi wa Kiteto kuhusu fursa za bomba la mafuta la EACOP, ambalo litapita wilayani hapo, leo Juni 6,2023.
Sehemu ya washiriki wa semina wakifatilia elimu iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa wafanyabiashara, mafundi watoa huduma na wananchi wa Kiteto kuhusu fursa za bomba la mafuta la EACOP, ambalo litapita wilayani hapo, leo Juni 6,2023.
Mkuu wa Wilaya Kiteto, Mhe Mbarak Batenga( katikati aliyeketi),akiwa katika picha ya pamoja Kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mha. Lorivii Long’ idu na kulia ni Amani Lechipya, mwakilishi wa Meneja wa TANESCO, Wilaya Kiteto. Wengine ni viongozi wa washiriki wa semina na watumishi wa EWURA, mara baada ya ufunguzi wa semina kuhusu fursa za bomba la mafuta la EACOP, leo Juni 6,2023.
Na.Mwandishi Wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,Mhe. Mbarak Batenga, leo 6 Juni 2023 amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga ( EACOP), ambalo litapita wilayani hapo.
Akifungua semina ya EWURA kwa wafanyabiashara, mafundi, watoa huduma na wananchi wa Kiteto kuhusu kuzitambua fursa na namna ya kujisajili kwenye kanzidata ya EWURA, Mhe. Batenga amewasishi wadau hao kuhamasika kujisajili ili waweze kutoa huduma na utaalamu kwenye mradi huo wa EACOP.
EWURA huwasajili bila malipo kwenye kanzidata https://cqs.ewura.go.tz/
watanzania wenye sifa ya kutoa huduma mbalimbali kwenye miradi ya mafuta na gesi asilia nchini.