Featured Kitaifa

DC SHEKIMWERI AZIONYA KAMPUNI ZA USAFI KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Written by mzalendoeditor
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi mara baada ya kufanya  usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akifanya usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Dkt. Andrew Komba wakifanya usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
Viongozi na wanafunzi mbalimbali kutoka Vyuo mbalimbali wakifanya usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi mara baada ya kufanya  usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Dkt. Andrew Komba,akizungumza mara baada ya kufanya  usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, Dkt. Tumaini Haonga,akizungumza mara baada ya kufanya  usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika kata ya Ipagala leo Juni 4,2023 jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya  siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5, mwaka huu.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amezitaka kampuni za usafi zilioingia mikataba na Jiji la Dodoma kutimiza wajibu wao kikamilifu wa kuondosha taka kulingana na mikataba waliyoingia ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Shekimweri,ameyasema hayo leo Juni 4,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na wananchi  mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi lililofanyika katika kata ya Ipagala ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika kesho Juni 5,mwaka huu.

Shekimweri amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma kuhakikisha anasimamia vikundi vya usafi pamoja na makampuni ili yatekeleze majukumu yao kama mikataba yao inavyoelekeza.

“Siyo jambo la busara sisi kwenda kufanya usafi katika maeneo ambayo kuna vikundi na makampuni ua usafi ambayo yameingia mikataba na kulipwa fedha nyingi na serikali”amesema DC Shekimweri

Aidha amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi wakati wote badala ya kuendelea kusubiri wakati wa maadhimisho.

“Lazima tujenge tabia ya kufanya usafi wakati wote siyo kusubiri wakati wa maazimisho kama haya na kupiga picha na kuposti inatupasa tuendele kuwa na tabia ya kufanya usafi katika maeneo yetu kila siku”amesema 

Hata hivyo  Shekimweri,ameuagiza uongozi wa halmashali ya jiji la Dodoma kuzitumia sheria ndogo zilizopo kuwachukulia hatua watu ambao wamekuwa wakifanya uchafuzi wa mazingira.

“Zipo sheria ndogondogo za halmashauri ambazo zinawabana watu wanaofanya uchafuzi wa mazingira nawaomba mzitumie ili kukomesha vitendo  hivyo lakini pia itakuwa chanzo cha mapato kupitia faini zilizopo kwa mujibu wa sheria”amesema

Aidha, amewahimiza viongozi wa kata na mitaa kusimamia kauli mbiu za utunzaji wa mazingira zilizopo kwa vitendo ikiwemo ya usafi mita tano,mita tano usafi wangu ili jamii ijenge tamaduni za kufanya usafi katika maeneo yao

“Watendaji wa mitaa na kata piteni katika maeneo yenu mhamasishe watu kufanya usafi lazima tuhakikishe uchafu wote uliopo katika maeneo yetu unaondoshwa wote”amesisitiza

Hata hivyo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanafanya usafi kwenye maeneo yao ya biashara kama ambavyo miongozo mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na wizara ya afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Dkt. Andrew Komba amesema kauli mbiu ya mwaka huu imejikita kwenye kupinga matumizi ya plastiki kutokana na bidhaa hiyo kuwa na  madhara kwa viumbe hai na mazingira.
“Tukiamua Kwa pamoja kuachana na matumizi ya vifungashio na mifuko ya plastiki pamoja na utupaji wa taka ngumu katika mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua tutayaweka Mazingira yetu katika Usalama na Mazingira yakiwa safi na salama hata Afya zetu zitakuwa salama,”amesema Dkt.Komba
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, Dkt. Tumaini Haonga ,amewahimiza wananchi kufanya usafi wa mara kwa mara ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. 
“Niwahimize  wananchi  kudumisha Usafi wa Mazingira kwani ni tunu ya Afya zetu kwani Mazingira yakiwa machafu ni hatari sana Kwa Afya zetu na viumbe vinavyotuzunguka kwani ni njia salama ya kuepukana na Magonjwa ya Mlipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na magonjwa yasiokuwa ya kuambikiza kama Saratani”amesema Dkt.Haonga

About the author

mzalendoeditor