NAIBU waziri wa Kilimo Antony Mavunde, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki kufanya usafi wa mazingira jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Juni 5, mwaka huu leo Juni 2,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde (katikati) akifanya usafi wa kusafisha mtaro wa maji katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama akifanya usafi wa kusafisha mtaro wa maji katika eneo la Makore Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa Juni 2, 2023 ) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Godwin Gondwe wakifanya usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde akiongozana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Mhe. Godwin Gondwe wakati wa zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Nyuma ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.
Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Bi. Fatma Mganga akitoa salamu za ukaribisho kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Maunde wakati wa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,mara baada ya kushiriki kufanya usafi wa mazingira jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Juni 5, mwaka huu leo Juni 2,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama,akizungumza mara baada ya kushiriki kufanya usafi wa mazingira jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Juni 5, mwaka huu leo Juni 2,2023 jijini Dodoma.
SERIKALI imewakemea wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaoendelea kuingiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa za plastiki zisizokidhi viwango zinazotumika kama vifungashio ambavyo zimekuwa chachu ya uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza katika zoezi la usafi wa mazingira katika kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu leo Juni 2, 2023 Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amesema ni wajibu wa Wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za Serikali katika kusimamia usitishaji wa Matumizi ya bidhaa za plastiki.
“Kumekuwa na juhudi mbalimbali za Serikali na wadau katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki, hata hivyo bado kuna ukwiukwaji wa sharia kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoingia na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango ambayo inayotumika madukani na watoa huduma” amesema Mhe. Mavunde.
Mhe.Mavunde amewaka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kudhibiti matumizi ya mifuko na bidhaa za plastiki kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaaa ili kkurahisisha zoezi hilo la kutokomeza vifungashio visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa visambazwa kupitia njia za panya.
Aidha Mavunde amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhamasisha suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya miji mikuu nchini ikiwemo Jiji la Dodoma, hivyo ni wajibu wa wananchi kuwataka wakazi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla kutosubiri Kilele cha Maadhimisho ya mazingira katika kujishughulisha na suala la usafi katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Mavunde amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku kwa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na salama kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, aamewataka wanasiasa kuacha kutumia vibaya nafasi zao kuchochea wananchi kuharibu mazingira.
“Maji ya mji wa Dodoma kwa asilimia kubwa yanatoka kwenye msitu wa Chenene hivyo kama wanasiasa wataweka siasa kwenye suala la mazingira tutapata shida sana kwani msitu huu ndiyo unachangia maji ya mkoa wa Dodoma kwa asilimia 70”amesema Bw. Gondwe
Aidha amesema kuwa hivi sasa dunia ikabiliana na mabadiliko tabianchi ambayo yamekuja na athari nyingi ikiwemo kukauka kwa vyanzo vya maji, uhaba wa mvua hali ambayo inachangia mifugo kukosa malisho pamoja na maji.
Awali Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama amesema Ofisi hiyo imejipanga kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma hatua inayolenga kupendezesha taswira ya Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya Serikali.
Kuanzia jana Juni Mosi ambayo tulizindua Wiki ya Mazingira tumeanza kwa kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma. Zoezi hili litaendelea hadi siku ya Kilele Siku ya Jumatatu Juni 5 mwaka huu” amesema Dkt. Mkama.