Featured Kitaifa

KATAMBI ATAKA UBUNIFU WA MAWASILIANO OFISI YA WAZIRI MKUU

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa mpango wa pamoja wa mawasiliano wa ofisi hiyo pamoja na taasisi zake kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mkoani Arusha tarehe 1 Mei, 2023.

Sehemu ya Wakuu na Maafisa wa Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mkoani Arusha tarehe 1 Mei, 2023.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ibrahim Hamidu akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Said Mabie akitoa elimu kuhusu Mpango Mkakati wa Ofisi hiyo pamoja na taasisi zake wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mkoani Arusha.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bi. Laura Kunenge akichangia jambo wakati wa kikao kazi hicho kilicholenga kuandaa mpango wa pamoja wa mawasiliano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Taasisi zake.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu na Maafisa wa vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano baada ya kufungua kikao kazi cha kuandaa mpango wa pamoja wa mawasiliano wa ofisi hiyo pamoja na taasisi zake kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mkoani Arusha tarehe 1 Mei, 2023.

Na: Mwandishi Wetu

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amewataka Wakuu wa Vitengo na Maafisa Mawasiliano wa Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake kuwa wabunifu na kuongeza wigo wa kujitangaza.

Mhe. Katambi ameyasema hayo Juni 1, 2023 jijini Arusha katika kikao kazi cha kuandaa mpango wa pamoja wa mawasiliano kati ya Ofisi hiyo na taasisi zake ambazo ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Naibu Waziri Katambi amesema vitengo vya mawasiliano vinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia na kuja na ubunifu utakaorahisha kufikisha taarifa muhimu kwa umma.

Pia, ameelekeza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo na Wakurugenzi wa Taasisi hizo kuangalia umuhimu wa kuongeza bajeti kwa vitengo hivyo ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Said Mabie na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo, Ibrahim Hamidu wameeleza madhumuni ya kikao hicho na umuhimu wa kuwa na mpango huo katika kusaidia kuwa na uratibu mzuri wa kufikisha taarifa kwa umma.

About the author

mzalendoeditor