Featured Kitaifa

UMEME JUA KUANZA KUZALISHWA NCHINI NA KUINGIZWA KWENYE GRIDI YA TAIFA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia utiaji saini mkataba wa kwanza nchini wa kuzalisha umeme wa jua kwa kutumia teknolojia ya “Solar Photo Voltaic” kati ya TANESCO na “SINOHYDRO CORPORATION” kutoka China wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150 za umeme hafla iliyofanyika leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia utiaji saini mkataba wa kwanza nchini wa kuzalisha umeme wa jua kwa kutumia teknolojia ya “Solar Photo Voltaic” kati ya TANESCO na “SINOHYDRO CORPORATION” kutoka China wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150 za umeme hafla iliyofanyika leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nishati Mhe. January Makamba,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka,,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika  la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw.Maharage Chande,akitoa taarifa ya mradi wa umeme Jua katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa  hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Judith Kapinga,akizungumza wakati wa  hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe.Boniphace Nyangindu Butondo,akiipongeza Serikali kwa hatua hiyo wakati wa  hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,akiishukuru serikali kwa mradi huo ambao unakwenda kujibu kero ya kukatika kwa umeme katika mkoa wake wakati wa  hafla ya utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya wageni waalikwa wakifatilia utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nishati Mhe. January Makamba,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji  saini wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa mara ya kwanza nchini wenye uwezo wa kuzalisha Megawati  50 katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika .leo Mei 29,2023 jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA WILSON JOHN

Na Neema Mbuja, DODOMA

Shirika la umeme Tanzania TANESCO leo kwa mara ya kwanza limeweka historia  kwa kusaini mkataba wa kwanza wa  kuzalisha umeme kwa wa  njia ya jua kwa teknolojia ya “Solar Photo Voltaic”  ambapo jumla ya megawati 50  zitazalishwa. 

Mradi huu mkubwa kuwahi kutokea wa kuzalisha umeme kwa kutumia jua hapa nchini na katika ukanda wa Afrika mashariki utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza zitazalishwa megawati 50 Kutoka wilaya ya Kishapu mkoani shinyanga na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika Mei 29, 2023 mjini Dodoma ambapo ilishuhudiwa na waziri wa Nishati Mhe. January Makamba ambapo aliipongeza TANESCO kwa hatua iliyofikia kupatikana kwa mkandarasi na hatimae kusainiwa kwa mkataba huo ambao utagharinu kiasi Cha shilingi bilioni 275 pindi utakapokamilika .

Mhe. Makamba amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia Nishati jadidifu  kwa Sasa WIZARA inaandaa mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa TANESCO inafanya upembuzi yakinifu na kuainisha maeneo ambayo yanafaa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vya Nishati jadidifu.

“Serikali kupitia WIZARA ya Nishati inakamilisha mpango mkakati wa uwekezaji kwenye maeneo haya kwani kwa sasa yanapewa kipaumbele sana kwenye uzalishaji wa umeme na naiagiza TANESCO itengeneze mwongozo unaoonyesha maeneo yote yanayofaa kwa uwekezaji kwa kutumia Nishati jadidifu” alisema Makamba

Akizungumza juu ya mradi huo wa kuzalisha umeme kwa njia ya jua mkurugenzi mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza utazalishwa megawati 50 na awamu ya pili megawati 100 na utatekelezwa na kampuni ya SINOHYDRO CORPORATION kutoka nchini China.

Maharage amesema kusainiwa kwa mkataba huu ni sehemu ya mpango wa mapinduzi katika kuzalisha umeme kutumia vyanzo mbadala ukiacha vile vya maji,na gesi nchini ili kufikia lengo la kuwa na Megawati 5000 kwenye gridi ya taifa ifikapo 2025. 

Utekelezaji wa mradi huo unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mkopo uliotolewa na Shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD) unatarajiwa kuanza mwezi juni 2023 ambapo utachukua miezi 14 hadi kukamilika kwake. 

Utiaji saini Mkataba huu ulishuhudiwa na Waziri wa Nishati Mhe January Makamba,Naibu waziri wa Nishati Mhe Stephen Byabato, mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,Waheshimiwa wabunge viongozi waandamizi wa wizara na  menejimenti ya TANESCO waliohudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa Morena ulioko Mkoani Dodoma. 

About the author

mzalendoeditor