Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2023 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Mipango wa Mwaka, 2023 (The Planning Commission Bill, 2023) na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali yatokanayo na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 (The Laws Revision (Miscellaneous Ammendments) Bill, 2023) kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.
Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 27 – 28 Mei, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Utawala, Katiba na Sheria, Ghorofa ya 5 Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Miswada hiyo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Vilevile itapokea maoni kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941,
41105 Tambukareli,
DODOMA.
Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz
Muswada huo pia unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
24 Mei, 2023.