Featured Kitaifa

WAKURUGENZI WA BODI  CPB WAPIGWA MSASA NA  IoDT

Written by mzalendoeditor

 

Katikati mbele ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CPB Salum Awadh akiwa katika mafunzo ya Utawala Bora yanayoendeshwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)

NA MWANDISHI WETU,MWANZA.
WAKURUGENZI wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wamepigwa msasa kwa kupatiwa mafunzo ya kiuongozi ya Utawala Bora na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania( IoDT) yanayoendelea Jijini Mwanza.
Aidha Wakurugenzi hao ambao huu ni mwaka wa pili tangu wateuliwa wameeleza kuwa mafunzo hayo waliyopata yatasaidia kuongoza b hiyo kwa weredi na ufanisi mkubwa ikiwana na lengo la kukuza Uchumi wa Nchi na mtu mmoja mmoja.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CPB Salum Awadh alisema kuwa wamefurahi kupatiwa mafunzo hayo kwani wanaamini wanaenda kufanya kazi kwa mafanikio makubwa.
‘’Kwenye mashirika ya umma kuna changamoto za kiungozi ya kusimamia mali za umma, hivyo ukiwa na uwezo mdogo huwezi kusimamia rasilimali, kwa hiyo mafunzo haya yatasaidia wakurugenzi wa Bodi kuelewa mipaka yao na kukabiliana na changamoto za kiungozi’’, alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema haya mafunzo yanasaidia kuonesha mipaka kati ya Bodi na Menejment hivyo mafunzo haya yamekuja wakati muhafaka katika uongozi huo mpya ili waweze kuonesha mabadiliko.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema awali Bodi hiyo ilikuwa ikifanya kazi zake kwa ufanisi mdogo lakini katika msimu huu Bodi hiyo imepanga kuboresha ufanisi wake kwa kuchakata mazoa zaidi ya tani 200.
Mwenyekiti huyo alisema katika kipindi cha nyuma katika upande wa viwanda walikua hawafanyi vizuri hivyo sasa wamejipanga kufanya kwa ufanisi kutoka asilimia 30 hadi kufikia asilimia 70.
Naye mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo Kapenjama Ndile aliongeza kuwa mafunzo haya yatawasaidia kuendesha mashirika ya umma kwa kuongeza uwezo wa kiulewa wa namna ya kuendesha mashirika ya umma hasa katika sekta ya Kilimo.
‘’Tuko hapa Mwanza leo siku ya Tano tunanolewa na magwiji wa mafunzo tunaamini wazi tukitoka hapa tunaenda kufanya mapinduzi makubwa ya kiungozi katika Bodi ya CPB’’, alisema Ndile ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea
Aidha Ndile alisema kuwa Bodi hiyo ipo kwaajili ya kuwasaidia Wananchi na kukuza Uchumi wa Nchi hivyo Taasisi yao itanunua mazao mengi na kuyachakata katika Viwanda vya CPB .
‘’Mafunzo haya yamenisaidia kuelewa kumbe Shirika la umma linaweza kujiendesha bila kulalia wakulima lakini kujiendesha kiushindani, kupata bidaa zilizo bora ambazo unaweza kuzitafutia masoko popote Duniani.’’, alisema Ndile.
Aidha Halima Dendego ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Bodi hiyo alisemamafunzo haya yatawasaidia kujiimarisha kimta katika kuhakikisha wanapata ujuzi ili wajiendeshe kiushindani.

‘’Mbinu ya kwanza ni wewe mwenyewe ujue unafanya katika wakati gani, kujua washindani wako pamoja na kujiimarisha kimtaji hivyo vyoote vinakupeleka kufanya vizuri katika kazi’’, alisema Dendego
‘’Sisi tumekuja kimkakati mpya tumekuwa kama kiungo katika ya Wakulima na Serikali, niwahakikishie Wakulima na wafanyabiashara wa mazao CPB iko vizuri na kukuhakishia watakaofanya kazi na sisi watapata hela zao kwa haraka’’, alisema Dendego ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Taasisi ya IoDT imekuwa ikitoa mafunzo katika kipindi cha wiki Nzima Jijini Mwanza kwa Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za umma wakiwemo Wakurugenzi wa Bodi ya CPB, ambao wamepatiwa mafunzo ya uongozi na Utawala Bora.
CPB ni Shirika la Umma la Kibiashara lililopo Chini ya Wizara ya Kilimo ambalo ununua mazao kutoka kwa Wakulima na wafanyabiashara wa Mazao na kuyaongezea thamani kwa kuyachakata katika viwanda vyao vilivyopo katika baadhi ya Mikoa Nchini.

About the author

mzalendoeditor