Featured Kitaifa

VIDEO:MBUNGE KAMAMBA AHOJI USAWA KATIKA SERA YA ELIMU.

Written by mzalendoeditor

 

Mbunge wa Jimbo la Buyungu,Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mhe.Aloyce Kamamba amehoji juu ya usawa uliopo kati ya Mwanafunzi wa Kike na Kiume chini ya Sera ya Elimu isemayo mwanafunzi akikaa nje ya shule kwa Siku 90 tayari ameshajiondoa kwenye Mfumo wa Elimu.

 

Ambapo amehoji “Sera hiyo haitoi haki sawa kwani wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wameruhisiwa kurudi huku wanafunzi wa Kiume wanaopata changamoto mbalimbali na kushindwa kuhudhuria masomo kwa siku 90 wanafutwa kwenye Mfumo wa Elimu ,Je usawa upo wapi wakati yule wa kike anakaa zaidi ya miezi tisa nyumbani? 

 

Pia Mhe.Kamamba ameitaka wizara ya Elimu kuja na Takwimu juu ya wanafunzi wangapi wamepata ujauzito wakiwa Shuleni na kurudi tangu Mhe.Rais Dkt.Samia aliporuhusu hivyo.

 

“Pia nataka kufahamu hizo changamoto zinazowakumba hao wanafunzi mpaka wanapata Ujauzito mnazishughulikiaje? ,”Ameuliza Mhe.Kamamba Wakati akichangia Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Mei 16,2023 Bungeni Jijini Dodoma

About the author

mzalendoeditor