Featured Kitaifa

CCM ZANZIBAR YAGUSWA NA KASI YA DK.MWINY

Written by mzalendoeditor

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinampongeza kwa dhati Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,kwa kukamilisha kwa mafanikio makubwa ziara yake ya kichama katika Mkoa wa Mjini.

Katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi,amekutana na kuzungumza na Viongozi wa ngazi za Mashina(Mabalozi) Matawi, Wadi, Majimbo, Wilaya hadi Mkoa pamoja na kukagua miradi ya Chama na Jumuiya zake hatua ambayo ni sehemu ya kiutendaji katika misingi ya kuimarisha  Chama.

Kasi ya kiutendaji ya Rais Dk.Mwinyi, ni kielelezo tosha cha maendeleo endelevu ya kuifikisha Zanzibar kuwa miongoni mwa nchi chache za Visiwa zilizoendelea kiuchumi,kijamii,kiutamaduni na kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi, kinaamini kuwa dhamira,mipango,mikakati na dira za Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi aliyoitoa katika ziara yake ya Kichama katika Mkoa wa Mjini ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2020/2025.

Katika maelezo yake  Rais Dk.Mwinyi,amewahakikishia Wana CCM kuwa ataimarisha miundombinu ya kiuchumi ndani ya CCM ili iwanufaishe wanachama wote.

Sambamba na hayo, CCM Zanzibar itaunga mkono dhamira ya itaendelea kuthamini juhudi za Rais Dk.Mwinyi ya kutekeleza kwa vitendo llani ya CCM,  ibara ya 136 kifungu kidogo cha (c) kinachoelekeza kuzalisha ajira 300,000 kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ifikapo mwaka 2025.

NDG.KHAMIS MBETO KHAMIS,

KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI,

CCM ZANZIBAR.

About the author

mzalendoeditor