Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga (Kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF ) (kulia),Justina Mashiba wakitia Saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini baina ya UCSAF na watoa huduma za mawasiliano iliyofanyika Leo Mei 13,2023, Jijini Dodoma.
Na.Blogas Odilo-DODOMA
SERIKALI kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kujenga minara 104 kwenye Kata 104 maeneo ya vijijini na kueleza kuwa huduma hiyo itaboresha mawasiliano na kuwa kichocheo katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Hayo yamesemwa leo Mei 13,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga mara baada ya Hafla ya Kutia Saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini baina ya UCSAF na watoa huduma za mawasiliano nchini.
Mhandisi Ulanga amesema kuwa kwenye zabuni hizi za Leo ambazo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imesaini na Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) imewaongezea maeneo mengine 104 mbali ya yale maeneo 130 ambayo Shirika hilo ni mtoa huduma pekee Kwa sasa.
Amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na watoa huduma wengine wa mawasiliano ili kuhakikisha mawasiliano yanakuwa Bora Huku akibainisha kuwa hata kule ambako hawajashinda zabuni watashiriki kuboresha huduma zao.
“Najua Kuna maeneo hatujashinda zabuni ila hata kama hatujashinda sisi ni watoa huduma Kwa wananchi hivyo tutashirikiana kuweka mitambo yetu na sisi ili kuboresha huduma zetu kwani tunapaswa kuchochea maendeleo katika uchumi wa kidijitali”amesema Mhandisi Ulanga
Hata hivyo Aida, Mhandisi Ulanga amefafanua kuwa katika zabuni hiyo Serikali imewapatia ruzuku ya Bilioni 5 ambapo nao kama Shirika wataongeza kuhakikisha Ujenzi wa monara hiyo inakamilika ili wananchi waishio maeneo ya vijijini waanze kupata huduma.
Mhandisi Ulanga amesema huduma za TTCL zinapatikana kila palipo na ofisi za Shirika
la Posta na kuendelea kufanya maboresho ili kuhakikisha huduma linazotoa zinakidhi viwango kwa kuboresha mitambo na kuongeza vituo vya huduma kwa wateja.
Aidha amesema maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kuhakikisha kituo cha huduma kwa wateja (call center) kinakuwa thabiti na kupatikana ndani ya muda stahiki;
Mhandisi Ulanga amesema shirika linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia huduma ya mawasiliano na kutoa huduma ya njia ya mawasiliano (capacity service) na huduma ya
maunganisho (interconnect) nje ya nchi na kufanikiwa kutanua wigo wa huduma kwa wateja.