Featured Kitaifa

MAPINDUZI MAKUBWA KUFANYIKA CPB,BILIONI 100 ZATENGWA

Written by mzalendoeditor

 

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa CPB Kapenjama Ndile akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza kutembelea miradi ya CPB Mwanza

Bodi ya Wakurugenzi w CPB wakiangalia Mpunga unaotarajiwa kuchakatwa katika Kiwanda cha Mkuyuni Mwanza.

Kushoto mwenye koti Jeupe ni Afisa mdhibiti wa CPB akitoa Maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa CPB

Katikati aliyevaa ushungi ni Nasra Majio msimamizi wa Kiwanda akitoa Maelezo mbele ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CPB waliofanya ziara katika Kiwanda cha kuchakata Mpunga kilichopo Mkuyuni Mwanza

Katikakati ni Afisa wa CPB akitoa Maelezo kuhusu Kiwanda cha kuchakata Mpunga kilichopo Mkuyuni Mwanza
NA MWANDISHI WETU ,MWANZA.
BODI ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) imesema inaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla kwa kutenga Sh. Billioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mazao kutoka kwa Wakulima hapa nchini.
Aidha Bodi hiyo imetangaza fursa kwa wakulima wote nchini kulima mazao mengi msimu huu kwani Bodi hiyo inaenda kunu nua mazao hayo kwa wingi na kwa bei ya soko.
Akizungumza jana mara baada ya ziara ya bodi hiyo kutembelea miradi yao iliyopo Kanda ya Ziwa Mwaza mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi aliyeongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kapenjama Ndile alisema wanaenda kufanya mapinduzi makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika Shirika hilo.
‘’Tunaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla tunaenda kununua mazao ya zaidi ya Sh. Billioni 100 kutoka kwa Wakulima wa hapa nchini’’., alisema Ndile.
Aidha Ndile aliwataka wakulima hapa nchini wazalishe mazao mengi kwani CPB itanunua mazao hayo kwa bei ya soko hivyo inatoa fursa kwa Watanzania kuuza mazao yao katika Bodi hiyo ili waweze kujikwamua Kiuchumi.
‘’CPB ni kimbilio kwa Wakulima tunanunua mazao kutoka kwao, lakini tunaongezea mazao thamani kwa kuchakata mazao kupitia viwanda vyetu vilivyopo katika baadhi ya Mikoa’’, alisema Mkurugenzi huyo wa Bodi hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema kipaumbele cha kwanza ni chakula na usalama wa Chakula, ndio maana Serikali iliunda Bodi ya Nfaka na Mazao Mchanganyiko ili kuwe na usalama wa chakula.
Aidha Ndile alisema Bodi hiyo inaendelea kujenga viwanda ikiwemo Kiwanda cha kuchakata Muhogo kitakachojengwa katika Jiji la Mwanza na Kingine kitajengwa Handeni Tanga.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Bodi alisema kuwa wataendelea kupanua Viwanda vilivyopo na kuajili wataalamu wa viwandani lengo ni kupanua wigo wa uzalishaji ili waweze kuuza bidhaa ndan I ya nchi na nje ya nchi.
‘’Tuna viwanda Vingine vilivyomo Arusha ambapo kuna Kiwan da cha kuchakata Mahindi, Ngano, kiwanda kingine kipo Iringa kinachakata Mahindi na Dodoma kinachakata Mahindi Alizeti’, alisema Linde.
Naye Mjumbe wa Bodi hiyo Fadhili Ngajilo alisema kuwa kuwa Bodi hiyo imepania kuleta mabadiliko makubwa kwa Watanzania kwa kufungua milango ya biashara kupitia CPB.
Alisema kuwa hivi sasa Bodi hiyo imetengeneza utaratibu wa kuwatambua madalali wa mazao kama wafanyabiashara rasmi kwaajili ya kurahisisha biashara kati ya wakulima na Bodi hiyo.
‘’Bodi hii imeingia kwenye ushindani wa biashara kwa kufanya biashara na mataifa ya nje ila tutaboresha kwa viwango vya Kimataifa’’, alisema Ngajilo.
David Shambwe ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo alisema kuwa wakulima walime mazoa mengi Bodi ipo kwajili yao kwani pia kutakuwa na mikata ya wakulima.
‘’Mikataba ya wakulima ina faida kubwa kwa wakulima kwa wanaweza kupata hata mikopo kutoka katika taasisi za fedha kwani watakuwa na vielelezo na mikata inayotambulika’’, alisema Shambwe.
Alisema Kuwa mikataba hiyo ipo kwenye mazao mbalimbali ikiwemo wakulima ya Ngano, Mahindi, Mpunga, Alizeti, ambapo alisistiza Vyama Vya msingi vihamasishe wakulima kulima mazao mengi soko lipo CPB.
CPB ni Shirikala la Kibiashara la serikali lililopo chini ya Wizara ya Kilimo kazi yake kubwa ni kununua mazao kutoka kwa Wakulima na wafanyabiashara wa mazao alafu wanayaongezea thamani kwa kuchakata katika viwanda vyao.

About the author

mzalendoeditor