WAWAKILISHI Pekee katika Kombe la Shirikisho barani Afrika Timu ya Yanga SC imejiweka nafasi nzuri ya kutinga Fainali ya Michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zikishambualiana kwa zamu na kupekeleka kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Yanga SC walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 64 Stephane Aziz Ki alianza kuitanguliza Yanga Sc mbele baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tusila Kisinda
Akitokea benchi kiungo Mtukutu Benard Morrison alipigilia msumari wa pili katika dakika za jioni kabisa 90+2′ .
Timu hizo zinatarajia kurudiana mechi ya Mkondo wa Pili May 17, 2023 nchini Afrika Kusini