Kaimu Meneja,TMDA Kanda ya Kati,Bw. Benedict Brashi,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Nelson Bukuru,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo Mei 10,2023 jijini Dodoma.
Meneja TMDA Kanda ya Kati Bi.Sonia Mkumbwa,akielezea lengo wakati wa mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo Mei 10,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo Mei 10,2023 jijini Dodoma.
Mfamasia kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Flora Makenya,akipongeza TMDA kuandaa mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Nelson Bukuru,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo Mei 10,2023 jijini Dodoma.
Alex Sonna-DODOMA
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imewataka wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya kuhakikisha wanatoa dawa kwa usahihi katika hospitali na vituo vya afya.
Hayo yameelezwa leo Mei 10,2023 Jijini Dodoma na Kaimu Meneja,TMDA Kanda ya Kati,Bw. Benedict Brashi wakati wa mafunzo ya siku moja ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma.
Bw. Brashi amesema TMDA wana jukumu la kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba, vitendanishi pamoja na bidhaa za tumbaku.
Amesema udhibiti unaaanza na mahali ambako bidhaa zinatengenezwa mpaka maeneo ambayo zinauzwa.
“Tunafanya mafunzo wataalamu walio katika vituo vinavyotumia na kutunza dawa za tiba zenye asili ya kulevya kwa kuwa kama Nchi tuna miongozo ya udhibiti wa dawa hizi na sisi kama TMDA ndio wasimamizi wa miongozo hiyo.”
Amesema katika mafunzo hayo watapitishana katika muongozo wa TMDA ambao lengo lake la msingi ni kuhakikisha dawa hazitumiki ndivyo sivyo katika Hospitali na kwenye vituo vya afya.
“Kwa umuhimu huo tutahakikisha matumizi yake yanakuwa sahihi na kwa watu sahihi ili kuepusha athari zinazoweza kusababishwa na matumizi holela ya dawa hizo ikiwemo mwili kujenga utegemezi.” amesema
Awali akifungua mafunzo hayo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Nelson Bukuru, ameipongeza TMDA kwa kuandaa mafunzo haya ambayo ni muhimu kwa watumishi wa afya katika kusimamia na kudhibiti dawa za tiba zenye asili ya kulevya.
”Kushiriki kwenu kwenye mafunzo hayo kutawaongezea uelewa katika utoaji wa huduma ya dawa za tiba zenye asili ya kulevya hivyo elimu mtakayoipata itasaidia katika matumizi
sahihi ya dawa hizo.” amesema Dkt.Bukuru
Hata hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanayaishi katika utendaji kazi wao ili kuwezesha matumizi sahihi ya dawa hizi.
Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Flora Makenya amesema wamefurahi kushiriki mafunzo hayo na ana matarajio makubwa na elimu aliyoipata na atawafundisha wengine kuhusu matumizi sahihi ya dawa hizo.