Featured Kitaifa

MTATURU AIBANA SERIKALI UJENZI WA BARABARA

Written by mzalendoeditor

SERIKALI imemuhakikishia Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu kuwa itatekeleza ahadi yake ya kujenga barabara ya Singida – Kwamtoro-Handeni yenye urefu wa kilomita 462 kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema hayo Mei 10,2023,Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo.

Katika swali lake Mtaturu ametaka kujua ni lini mkandarasi ataenda kuanza kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

“Barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wan chi yetu kwa sababuulitambia tayariimeshawekwa kwenye mpango wa kujengwa na imetangazwa katika kilomita 2,100,ni lini sasa mkandarasi atakuja kuanza kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami,?”amehoji Mbunge huyo.

Akijibu swali hilo Kasekenya amesema serikali ina mpango thabiti wa kuijenga kwa kiwango cha lami.

“Nimuhakikishie mbunge kuwa mpango wa kuijenga barabara hii tunao na kama tulivyokuwa tunaelezea kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami,nimuombe mbunge avute subira ataisikia tutakapokuwa tunasoma bajeti yetu,

“Naomba mbunge usiwe na wasiwasi,serikali imeweka kwenye mpango wa IPC+F na itaonekana kwenye bajeti hii ya 2023/2024 itakayowasilishwa bungeni,” amesema.

Septemba 12,2019,Mtaturu kupitia swali lake la nyongeza kwa wizara ya ujenzi na uchukuzi aliomba kujua ni lini serikali itaanza ujenzi wa barabara Njiapanda kupitia Kwamtoro,Makiungu hadi Handeni ambayo ina umuhimu katika uchumi wa wananchi wa eneo hilo.

Aidha,Mei 17,2021,akichangia bajeti ya wizara hiyo pia aligusia barabara hiyo.

About the author

mzalendoeditor