Featured Kitaifa

ZAIDI YA SH.BILIONI 164 KUJENGA MRADI UONDOSHAJI MAJITAKA JIJI LA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso  akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya  usanifu wa ujenzi wa mradi wa majitaka katika jiji la Dodoma utakaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya  usanifu wa ujenzi wa mradi wa majitaka katika jiji la Dodoma utakaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi,akizungumza wakati wa utiaji saini kati ya DUWASA na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa utiaji saini kati ya DUWASA na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph,akitoa taarifa ya mradi huo wakati wa utiaji saini kati ya DUWASA na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Donald Mejiti,akizungumza wakati wa utiaji saini kati ya DUWASA na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis G. Mwamfupe ,akizungumza wakati wa utiaji saini kati ya DUWASA na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya  usanifu wa ujenzi wa mradi wa majitaka katika jiji la Dodoma utakaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na  kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea hafla iliyofanyika leo Mei 9,2023 katika Ofisi za DUWASA jijini Dodoma

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI  imesaini mkataba na kampuni ya Dohwa – Saman ya nchini korea kwa ajili ya mradi wa kuboresha huduma ya uondoshwaji  na kutibu maji taka katika jiji la Dodoma mkataba wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 164 ili kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo.

Akizungumza leo Mei 9,2023 jijini Dodoma mara baada ya kushuhudia Utiaji saini huo , Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa majitaka yasipowekewa utaratibu mzuri tunaingia katika eneo zima la uchafuzi wa Mazingira

Waziri Aweso amesema kuwa asilimia 20 ya wakazi wa Dodoma wanapata huduma ya uondoshaji majitaka ambapo katika ya wakazi hao kata 14 kati ya 41 ndio wanapata huduma ya majitaka kupitia mtandao wa DUWASA uliopo, ambao ufanisi wake hauendani na ongezeko la kasi la watu katika Jiji la Dodoma na uzalishaji wa Majitaka.

“Tunaambiwa kuwa Asilimia 80 ya Majisafi yanayotumika na binadamu katika matumizi yake ya kila siku hugeuka kuwa Majitaka sasa tujiulize yanakwenda wapi zaidi ya kwenda kuchafua Mazingira?,”amesema Aweso

Hata hivyo Aweso amekiri kuwa Wizara ya Maji hawajafanya uwekezaji wa kutosha katika eneo la uondoshaji wa Majitaki.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa kemikimba amesema kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dodoma kumesababisha  miundo mbinu ya majitaka kuelemewa hivyo usanifu ufanyike sambamba na kupatikana mkandarasi ili ujenzi wa mradi uanze.

Awali akitoa taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa gharama za mradi huo kwenye Usanifu na Ujenzi unategemea kugharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 70 sawa na Shilingi Bilioni 164.85 za Kitanzania.

Mhandisi Joseph amesema ,Mkataba wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huo utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 5,225,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 12.3

“Mradi huu unalenga kuhusisha Usanifu na ujenzi wa Mabwawa mapya makubwa 16 yenye uwezo wa kutibu takribani lita milioni 20 kwa siku,usanifu na ujenzi wa bomba kubwa (trunk main) kwa kilometer 107.5,ubadilishaji wa bomba chakavu kilomita 2.6 na ukarabati wa Kilomota 2.1 za Mtandao wa majitaka,”amesema Mhandisi Aron

Aidha Amesema ,Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha Miezi 49 ambapo awamu ya kwanza Mhandisi Mshauri atafanya kwa muda wa miezi 13 kusanifu Mradi na awamu ya atatumia miezi 36 katika ujenzi wa Mradi huo.

About the author

mzalendoeditor