HAUKUWA Msimu wa Mafanikio kwa Simba SC ndivyo unaweza kusema! baada ya kutupwa nje kwa mbao 2-1 na Azam FC katika hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) mchezo uliopigwa uwanja wa Nangwanda mkoani Mtwara.
Azam FC walianza kupata bao dakika ya 22 likifungwa na Lusajo Mwaikenda baada ya mlinda mlango wa Simba SC kuutema Mpira hata hivyo bao hilo halikudumu kiungo Mkabaji Sadio Kanout aliisawazishia Simba SC dakika ya 28 na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayo yaliinufainsha Azam FC mnamo dakika ya 74 Prince Dube alipachika bao la ushindi.
Kwa Matokeo hayo Azam FC imetinga Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2023 na sasa inasubiri Mshindi Kati ya Singida Big Stars au Yanga SC Fainali itkayopigwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.