Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWASILI WINDHOEK NCHINI NAMIBIA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA TROIKA PLUS

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC) tarehe 07 Mei, 2023. Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia kwa ajili ya mkutano wa Dharura wa TROIKA Plus utakaojadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tarehe 07 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Watoto Miranda Masatu wa kwanza kulia, pamoja na Samra Mdee mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia tarehe 07 Mei, 2023. Wa kwanza kulia ni Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob akishuhudia tukio hilo.

About the author

mzalendoeditor