Featured Kitaifa

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UONGOZI, MHITIMU KUTOKA TMDA AMSHUKURU MWAJIRI WAKE

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimtunuku Stashahada ya Uzamili ya Uongozi  (Postgraduate) Diploma in Leadership Roberta Feruzi Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA baada ya kuhitimu mafunzo ya uongozi katika Taasisi ya Ungozi Institute katika Mahafali yaliyofanyika Ijumaa Mei 5,2023 Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Roberta Feruzi Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akishuka jukwaani baada ya kutunukiwa  Stashahada ya Uzamili ya Uongozi  (Postgraduate) Diploma in Leadership katika Mahafali Taasisi ya Uongozi Institute yaliyofanyika Ijumaa Mei 5,2023 Mlimani City jijini Dar es Salaam.  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa Katika picha ya pamoja na wahitimu wa Taasisi ya Uongozi  Institute waliosimama mbele kushoto ni Roberta Feruzi  Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akiwa na wenzake baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi  (Postgraduate) Diploma in Leadership katika Mahafali Taasisi ya Uongozi Institute yaliyofanyika Ijumaa Mei 5,2023 Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimtunuku mmoja wa wahitimu w mafunzo hayo Niko Mkapa ambaye ni Mtoto waRais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa katika mahafali yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa hotuba yake katika mahafali ya Taasisi ya Uongozi Institute yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Ijumaa Mei 5,2023 jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Ikulu, Mululi Mahendeka akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika leo kwenye ukumbi waMlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena A. Said  akizungumza katika mahafali hayo.

Picha mbalimbali zikionesha wahitimu wa mafunzo hayo ya Uongozi yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.

Wanawake nchini wametakiwa kujiunga na mafunzo ya uongozi kupitia programu maalamu inayotolewa na Taasisi ya uongozi iliyonzisha na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani.

Akizungumza leo tarehe 5/5/2023 Jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Taasisi ya Uongozi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa ni vizuri wanawake wakajiunga na mafunzo ya uongozi ili kuleta tija katika kuongeza idadi ya viongozi nchni.

“Kuna idadi ndogo ya wanawake katika safu ya uongozi nchini ni vizuri wakasoma mafunzo hayo ili kukuza vipaji vyao kwa ajili ya kuleta usawa katika utekelezaji wa majukumu” amesema Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene amewapongeza wahitimu kwa kupata mafunzo ya uongozi jambo jambo linakwenda kusaidia kufikia malengo tarajiwa katika kuwafikia wananchi kwa kutoa huduma bora.

Amewataka kwenda kuwa viongozi bora na kutumia vizuri talanta zao ili kuleta maendeleo kwa Taifa.

“Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema ili tuendelee tunaitaji mambo manne ambayo ni watu, ardhi, siasa safi pamoja na uongozi bora” amesema Mhe. Simbachawene.

Amefafanua kuwa hali ambayo inawasukuma kuandaa viongozi bora kutokana na ongezeko la idadi ya watu, kwani matokeo ya sensa na watu mwaka 2022 inaonesha Tanzania ina jumla ya watu milioni 61.7.

Ameeleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu asilimia 3.2, hivyo kuna idadi kubwa ya watu “tunaitaji viongozi bora makini kwa ajili ya kumudu kusimamia rasilimali za Nchi”.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa mafunzo ya uongozi ni muhimu, huku akiwataka wahitimu kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo yao ya kazi.

“Mkakuze utawala bora wenye kufata haki, kanuni, miongozo na taratibu, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza uaminifu, kuimalisha utendaji wa kazi ili kumsaidia Rais ambaye amefungua milango mingi ya kimaendeleo” amesema Mhe .Simbachawene.

 Kwa upande wake Roberta Feruzi Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA ambaye ni mhitimu wa mafunzo hayo ya uongozi  amemshukuru sana mwajiri wake TMDA kwa kumpa fursa ya mafunzo hayo ya ngazi ya juu katika Uongozi.

“Mafunzo haya yamenijengea uwezo, maarifa na stadi za juu katika uongozi kimataifa. Ujuzi huu utaongeza chachu katika utendaji wangu wa kazi na hivyo kuleta tija katika ufanisi wa kazi. Utaboresha utendaji wa Taasisi na kusaidia kuharakisha maendeleo ya nchi kwa ujumla,”. Amesema Roberta Feruzi.

About the author

mzalendoeditor