Na. WAF – Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe ameipongeza timu ya Afya Clubu kwa kufanikiwa kuibuka washindi wa tatu mashindano ya uendeshaji wa baiskeli upande wa wanaume na mshindi wa tatu mchezo wa kuvuta kamba upande wawanawake katika mashindano ya Mei Mosi 2023 yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Dkt. Grace ametoa paongezi hizo leo jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya viongozi wa Afya Club kukabidhi vikombe vya ushindi walioupata katika michuano hiyo.
Aidha Dkt. Grace ameitaka Idara ya Utawala kuhakikisha wote walioshiriki kufanyikisha ushindi huo wanapewa zawadi kama motisha ya kuwahamasisha kufanya vizuri wakati mwingine.
Vile vile amemuagiza Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya kuhakikisha mshindi wa mashindano ya Beiskeli kwa upande wa wanawake anapatiwa Beiskeli mpya itakayomuwezesha kufanya vizuri katika mashindano mengine yajayo.