Featured Michezo

SIMBA SC YASHINDWA KUTAMBA UGENINI DHIDI YA NAMUNGO FC

Written by mzalendoeditor

SIMBA SC wameshindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Namungo FC mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Majaliwa Mjini Lindi.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Jean Baleke dakika ya 27 hata hivyo bao hilo halikudumu mnamo dakika ya 37 Hassan Kabunda aliisawazishia Namungo.

Mabao hayo yalizipeleka timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana moja moja.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo  mabadiliko hayo hayakuinufaisha timu yoyote na kugawana Pointi moja moja.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 64 wakiwa nafasi ya pili wakiwa wamecheza mechi 27 huku Yanga SC akiendelea kuongoza Ligi hiyo akiwa na Pointi 68 akiwa na mchezo mmoja.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaopigwa uwanja wa Liti wenyeji Singida Big Stars watawakaribisha mabingwa watetezi Yanga SC mchezo ukaopigwa majira ya saa kumi jioni.

About the author

mzalendoeditor