Featured Kitaifa

UCSAF KUBORESHA HUDUMA ZA UTANGAZAJI WA REDIO JAMII KATIKA MIKOA SABA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Katika kuwawezesha watanzania kupata maudhui ya maeneo yao, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) unatekeleza mradi wa kuboresha huduma za utangazaji katika mikoa saba nchini.

Kupitia mradi huo, UCSAF itajenga mnara mmoja kwa kila Halmashauri, ambapo mtoa huduma yeyote mwenye redio Jamii katika mikoa hiyo anaweza kufunga vifaa vyake vya utangazaji na kutoa huduma kwa jamii husika kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Mkataba wa ujenzi wa minara hiyo umetiwa saini na mara baada ya ujenzi kukamilika minara itakabidhiwa kwa Halmashauri husika kwa ajili ya uendeshaji.

Kwa kuanza maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Ileje, Mtama, Same, Kilindi, Mbulu na Rufiji.

About the author

mzalendoeditor