Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Adolf Mkenda ,akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 20,2023 jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya wiki ya ubunifu Tanzania 2023 yatakayoambatana na maonesho, yanayotarajia kuanza Aprili 24-28, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Adolf Mkenda ,akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 20,2023 jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya wiki ya ubunifu Tanzania 2023 yatakayoambatana na maonesho, yanayotarajia kuanza Aprili 24-28, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Na.Bolgas Odilo-DODOMA
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imesema maandalizi kwa ajili ya wiki ya Ubunifu Tanzania 2023 ,yanaendelea vizuri na mwaka huu kwa mara ya kwanza kutakuwa na washiriki kutoka nchini Afrika Kusini.
Hayo yamesemwa leo Aprili 20,2023 jijini Didoma na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya ubunifu Tanzania 2023 yatakayoambatana na maonesho, yatakayoanza kuanzia Aprili 24-28, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri Dodoma,
Amesema wiki ya ubunifu ni sehemu ya mikakati y Serikali katika kuongeza hamasa ya matumizi ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo ya kuharakisha Maendeleo ya uchumi.
“Wiki ya ubunifu pamoja na mambo mengine imekuwa ikiibua, kutambua na kuendeleza jitihada zinazofanywa na wabunifu na watumiaji wa bidhaa hizo na inatoa fursa kwa wabunifu, wavumbuzi, watunga sera, wadau wa maendeleo na washirika wengine kukutana kujadili sera kanuni na miongozo mbalimbali ,”amesema Prof.Mkenda
Amesema tangu mwaka 2019 Wizara kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikiendesha wiki ya ubunifu maarifu kama Makisatu kwa lengo la kuimarisha mfumo wa ubunifu hapa nchini.
Hata hivyo amesema bunifu 38 zilizoibuliwa kwenye Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), tayari zimeanza kuingia sokoni.
Amesema kupitia maadhimisho ya wiki ya wabunifu kitaifa watafiti na wabunifu hupata nafasi ya kuonesha kazi zao.
“Kwa mara kwanza kutakuwa na uwashiriki kutoka Afrika Kusini.Maadhimisho hayo yatahusisha Taasisi za vyuo vya juu,Mashirika na Makampuni,Veta na shule za sekondari,
Kwa mara ya kwanza safari hii tutakuwa na washiriki kutoka Afrika ya Kusini imeanza kuchukua sura ya kimataifa.”amesema Prof Mkenda.
Prof Mkeda amesema wiki ya Ubunifu Tanzania itatanguliwa na maadhimisho katika ngazi za mikoa na Halmashauri na itaratibiwa na kuendeshwa kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), program ya Funguo chini ya UNDP, Ofisi ya Rais, Tamisemi na wadau wengine.
Amesema Mikoa 17 itakayofanya maadhimisho hayo ni pamoja na: Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Kagera, Mara, Ifakara, Njombe, Mtwara, Kilimanjaro, Songwe na Unguja Magharibi
kupitia kumbi mbalimbali za ubunifu.
Hata hivyo Prof.Mkenda ametoa wito kwa taasisi, mashirika, wizara za sekta na wananchi kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya ubunifu Tanzania 2023.