Featured Kitaifa

WAZIRI MABULA AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA MAGEUZI SEKTA YA ARDHI

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akimkabidhi hati miliki moja ya wananchi waliohudhuria zoezi la ugawaji hati katika mradi wa kupanga, kupima na kumiliki ardhi eneo la TX kata ya Shibula wilaya ya Ilemela,

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi katika kata ya Shibula eneo la Tx wilaya ya Ilemela wakati wa zoezi la ugawaji hati miliko 570 kwa wananchi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha zilizotumika katika kuleta mageuzi ya kidigitali katika sekta ya ardhi

Akizungumza wakati wa ziara yake katika kata ya Shibula wilaya ya Ilemela Dkt Mabula amefafanua kuwa Rais Dkt Samia ametoa fedha nyingi kwaajili ya usimikaji wa mifumo ya kidigitali ambapo sasa mwananchi anaweza kupata ujumbe wa taarifa za ardhi kupitia simu yake ya mkononi na kurahisisha zoezi la umiliki wa ardhi, ulipaji wa kodi na kutatua migogoro ya ardhi kwa mtu zaidi ya mmoja kumili kiwanja kimoja

‘.. Katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt Samia ardhi imekuwa na mageuzi makubwa ambayo hayajawahi kutokea, Sasa hivi watu wanapata meseji za taarifa zao za ardhi kwenye simu, mifumo pia inarekebishwa hakutakuwa na uwezekano wa kiwanja kimoja kumilikiwa na watu wawili ..’ Alisema

Aidha Dkt Mabula akawaasa wananchi kuhakikisha wanajenga kwa kufuata taratibu ikiwemo kulipia kibali cha ujenzi na kuzingatia mpango kabambe wa matumizi ya ardhi kwa jiji la Mwanza

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala amemshukuru Rais Dkt Samia kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa sekta za afya, elimu na miundombinu huku akiwapongeza diwani wa kata ya shibula na mbunge wa jimbo hilo kwa ushirikiano wao na usimamizi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati

Swila Dede ni diwani wa kata ya Shibula ambapo mradi wa upimaji, upangaji na umilikishaji wa viwanja umetekelezwa, Ameishukuru Serikali kwa mradi huo huku akiomba kupunguzwa kwa gharama za fidia katika mradi huo

Jumla ya hati 570 zimeandaliwa na kugaiwa wananchi wa kata ya Shibula na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula

About the author

mzalendoeditor