Featured Michezo

SIMBA SC YAUNGURUMA PALE PALE ALIPOFIA YANGA NA AZAM FC

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

SIMBA SC wameendelea kuitafuta Yanga SC katika mbio za Ubingwa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Ihefu mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Highland Estates jijini Mbeya .

Mabao ya Simba yamefungwa na Mshambuliaji hatari Jean Baleke dakika ya 83 na 87 na kuvunja mwiko wa Ihefu wa kuendelea kuzifunga timu kubwa katika uwanja wao ambap Yanga na Azam zote zilipata kichapo huku Singida Big stars ikiambulia sare.

Kwa Matokeo hayo Simba SC imefikisha Pointi 60 ikiwa imecheza mechi 25 huku Yanga SC bado anaongoza Ligi akiwa na Pointi 65 akiwa amecheza mechi 24.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Yanga SC itakuwa kibaruani kucheza na Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera mchezo utakaopigwa uwanja wa Chamazi Complex Azam majira ya saa moja usiku.

About the author

mzalendoeditor