Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AVUNJA BODI YA TRC NA KUTENGUA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA TGFA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Aidha, Rais Samia  ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali  (TGFA), Mhandisi John Nzulule. 

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi  kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa  Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa  haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.  

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika  kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria. 

About the author

mzalendoeditor