VINARA wa Kundi D katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Yanga SC imepangwa na Rivers United kutoka nchini Nigeria katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo na itaanzia ugenini mchezo wa kwanza.
Yanga SC walimaliza nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 13 sawa na US Monastirienne,nafasi ya tatu imeshikwa na Real Bamako na TP Mazembe wakiburuza mkia katika kundi hilo.
RATIBA KAMILI
1.Young Africans V Rivers United.
2.Marumo V Pyramid.
3.Asec Memosa V Monastr .U
4.FAR Rabat V Usm Alger.