Featured Kitaifa

DKT.YONAZI AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka (katika), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi(kulia),Katibu Mkuu ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Adolf Ndunguru wakiwa katika Kikao cha Makatibu Wakuu cha nishati safi ya kupikia wakipitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033, kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijijini Dodoma.

Wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha nishati safi ya kupikia, wakipitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033, wakimsikiliza kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Makatibu Wakuu Katibu, ambaye pia ni Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi, kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti ya Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia wakimsikiliza Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Makatibu Wakuu Katibu, ambaye pia ni Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi, kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijijini Dodoma.

Na Zuena Msuya Dodoma,

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu kilicholenga kupitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wiki moja iliyopita Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.

Dkt.Yonazi ameongoza Kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijini Dodoma.

Dkt. Yonaz amesema kuwa kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maboresho na maelekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokutana  na Mawaziri na Naibu  Mawaziri Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.

Mara baada ya Makatibu Wakuu hao kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi safi ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 na Rasimu ya Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, itawasilisha kwa Waziri Mkuu tarehe 31 Machi 2023.

About the author

mzalendoeditor