TAASISI ya WAJIBU imetoa mafunzo kwa
waandishi wa habari na Asasi za Kiraia (AZAKI) namna ya kufanya
uchambuzi wa masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma.

Akizungumza
mbele ya wadau hao wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku mbili
jana Machi 29, 2023,jijini Dodoma Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi
ya WAJIBU, Jackson Mmary ameeleza hatua kwa hatua umuhimu wa kuwa na
wadau kutoka maeneo mbalimbali ili kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti
zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.

Amefafanua kuwa ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ambayo inahusu masuala ya fedha ni
nyenzo muhimu ya kufuatilia mipango ya Serikali Kuu ama Serikali za
Mitaa na taasisi za kiraia.

“Tumekuwa tukifanya uchambuzi wa
ripoti ya CAG peke yetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, sasa
tumeona kuna umuhimu wa kuwashirikisha wadau. Kwa muelekeo wa WAJIBU
tukasema ukitaka kwenda haraka nenda peke yako lakini ukitaka kwenda
mbali nenda na wenzako, kwa hiyo tukaona ni muda muafaka kuanza kwenda
na wenzako,” amesema Mmary na kuongeza:

“Miaka iliyopita
tulikuwa tunafanya uchambuzi halafu tunawaletea, sasa hivi tunataka
kuwaongeza ili sisi na ninyi tufanye uchambuzi kwa pamoja halafu
tukitoka hapa twende mbele. Kwa kufanya hivyo tutawezesha kujenga kwa
pamoja yale tuliyokuwa tunayachambua na kuwaletea.

Kwa hiyo hivi
sasa nanyi mtakuwa na uwezo wa kuchambua, kwa hiyo tutakuwa na nguvu
zaidi kwa sababu ya kuhusika sote kwa pamoja. Kingine kitatuongezea
mawanda ya uchambuzi kwani tumekuwa tukifanya uchambuzi kama sisi na
kama tulikuwa watu 20 hapa leo wapo zaidi ya 40.”

Kutokana na
uwezeshaji uliofanywa, kwa sasa amesema kutakuwa na macho mengine 80
zaidi yale yaliyokuwa yanafanya uchambuzi mwanzoni.

“Sisi WAJIBU
na ninyi kuanzia leo tukitembea kwa pamoja tutakuwa tumejijengea uwezo,
ninyi mtakuwa mmetujengea uwezo na sisi tunawajengea uwezo, kwa hiyo
tutaongeza uzoefu na hasa ninyi mnaofanya kazi mikoani katika
halmashauri.

Pia kuna mambo ambayo inawezekana tusiyaone namna
ambavyo yanaathiri jamii na kila mtu anahoji ndio maana hapa kuna redio
za jamii, magazeti ya kitaifa pamoja na kuna asasi za kiraia. Kwa hiyo
tukiweka huo mchanganyiko tutaongeza mawanda, uzoefu zaidi katika
kufanya uchambuzi wa mambo yanayoathiri jamii,” amesema Mmary.
Meneja
wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya WAJIBU, Jackson Mmary akizungumza
mbele ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo
mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa Mafunzo siku mbili yanayoendelea
jijini Dodoma yaliyohusu namna ya kufanya uchambuzi wa masuala ya
uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma,lengo mojawapo ikiwa ni
kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za
umma.

Baadhi
ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo
mbalimbali nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati
mafunzo yakiendelea.
Mmoja wa Wandishi wa habari akichangia jambo
katika suala zima la kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu
uwajibikaji wa fedha za umma.


Ofisa
Utafiti na Uchambuzi wa Fedha kutoka Taasisi ya WAJIBU Maureen Mboka
akieleza jambo mbele ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI)
kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa Mafunzo siku mbili
yanayoendelea jijini Dodoma yaliyohusu namna ya kufanya uchambuzi wa
masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma,lengo mojawapo
ikiwa ni kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa
fedha za umma.
Wakifuatilia
baadhi ya vitabu vinavyohusu Ripoti ya uwajibikaji vinavyoandaliwa na
Taasisi ya WAJIBU ikiwa ni sehemu ya kujengeana uwezo wa kuchambua
ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.Picha mbalimbali wakati wa Majadiliano wa mafunzo hayo yakiendelea


Ofisa
Mawasiliano wa Taasisi ya WAJIBU Hassan Kissena akitoa ufafanuzi wa
baadhi ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiibuliwa wakati wa majadiliano
kwenye mafunzo hayo yaliyowakutanisha Waandishi wa habari pamoja na
Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo mbalimbali nchiniPrevious articleTET, CHUO KIKUU SHANGHAI WAINGIA MKATABA WA UFUNDISHAJI SOMO LA HISABATI NCHINI
Next articleNAMIBIA YAVUTIWA NA TANZANIA INAVYOKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here