Featured Kitaifa

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YANOGA, WAIMBAJI MAARUFU WAENDELEA KUTAMBULISHWA

Written by mzalendoeditor


Na Mwandishi Wetu Michuzi TV

MAANDALIZI
ya Tamasha la Pasaka yanazidi kunoga baada ya mwimbaji mwingine mahiri
wa nyimbo za Injli nchini, Christopher Mwahangila kuthibitisha kushiriki
tamasha hilo linalotarajia kufanyika Aprili 9 mwaka huu kwenye viwanja
vya Leaders Club,Kinondoni  Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo
linatarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa
Injili nchini hasa wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani.

Akizungumza
leo mbele ya Waandishi wa Habari katika Ofisi za Msama Promotion ambao
ndio waandaaji wa tamasha hilo, Mwahangila ambaye amejizolea umaarufu
mkubwa kutokana na  nyimbo zake za Injili zikiwemo Mungu ni Mungu,Fungua
Milango,Moyo Furahi,Yesu yuko hapa na nyinginezo amesema tamasha la
pasaka limekuja wakati muafaka kwani wamelikosa kwa  miaka mingi.

Amefafanua
miaka saba  imepita sasa bila kufanyika tamasha hili, hivyo
wanawashukuru waandaaji wa tamasha hilo ambao ni Msama Promotion kwa
kulirudisha tena mwaka huu,hakika ni jambo la kumshukuru Mungu huku
akisisitiza yuko tayari na amejipanga vema kwa ajili ya tamasha la
Pasaka.

“Tamasha la Pasaka litakonga nyoyo za waumini mbalimbali
wa nyimbo za Injili na nitaimba ‘live’ usipange kukosa, lakini pia
tujitokeze katika kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani
ya miaka miwili, njooni tusifu kwa pamoja,” amesema.

Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha
mbalimbali ya Injili nchini, Alex Msama amesema tamasha la mwaka huu
litakuwa la kihistoria na kufanyika bure.

Ameongeza maandalizi ya
tamasha la Pasaka yanaendelea vizuri na kwamba awali tamasha hilo
lilitakiwa lifanyike uwanja wa Taifa, lakini kwa sababu zilizo nje ya
uwezo wao  tamasha hilo litafanyika Leaders club.

“Kwa hiyo
tamasha lipo kama kawaida Aprili 9, 2023 na mpaka sasa waimbaji wengi
wamethibitsha kushiriki” amesema Msama na kuongeza tamasha  hilo pia
litakuwa la kumshukuru Mungu katika kusherehekea miaka miwili ya uongozi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan.Tutatumia  nafasi hiyo kumuombea ili aendelee kuiongoza nchi ya
Tanzania kwa amani.”

Pia tamasha hilo litakuwa la kumshuru Mungu
kwaajili ya uongozi wa mama yetu , Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza
miaka miwili madarakani kwa mafanikio makubwa, miradi mingi imeendelea,
kila kitu kinaenda vizuri, tunaishi kwa amani na utulivu hivyo ni
lazima tumshukru Mungu kwa uongozi wa Rais wetu” ameongeza Msama.

Kuhusu
waimbaji ambao watashiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na  mwimbaji
mahiri wa nyimbo za kusifu na kuabudu Upendo Nkone, kundi la Zabron
Singers Emmanuel na wengine wengi ambao wanaendelea kutangazwa.

Wakati
huo huo Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa amesema waimbaji
wote walioalikwa kushiriki kwenye tamasha hilo wamethibitisha ushiriki
wao na kwamba maandalizi yote yanaenda vizuri.”Tamasha hili lilikuwa
likisubiriwa kwa muda mrefu.

“Lakini kwa sasa limewadia, hivyo
niwaombe  wananchi wasisite kutoka na familia zao kuhudhuria kwenye
tamamsha hilo vyakula na vinywaji vitakuwepo kwa bei nafuu amesema
Mabisa.”

 

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka kila mwaka
Alex Msama (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika
bure bila kiingilio April 9, 2023 katika Viwanja vya Leders Club Jijini
Dar es salaam.

Mratibu wa tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa (kulia) akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya Tamasha hilo.

 

 

Mwimbaji
mahiri wa Nyimbo za Injili Christopher Mwahangila (pichani kushoto)
akiimba moja ya wimbo wake mbele ya waandishi wa habari kuonesha namna
alivyojiandaa kutumbuiza kwenye Tamasha la pasaka linalotarajiwa
kufanyika bure katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni,Jijini
Dar,kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha
hilo kila mwaka Alex Msama, akifurahi jambo.

About the author

mzalendoeditor