Featured Kitaifa

TAHA YAENDELEA KULETA MINYORORO YA THAMANI YA MAZAO YA HORTICULTURE KWA WAKULIMA WADOGO.

Written by mzalendoeditor

 

WAKULIMA wa zao la wakati wakivuna zao Hilo ( picha kutoka katika tovuti ya TAHA)

Meneja wa miradi na maendeleo wa asasi kilele inayojishulisha na mazao ya mboga mboga, matunda, viungo na mazao yatokanayo na mizizi TAHA, Antony Chamanga 

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Asasi kilele inayojishulisha na mazao ya horticulture yaani  mboga mboga, matunda, viungo na mazao yatokanayo na mizizi(TAHA) imeendelea kuleta minyororo ya thamani katika mazao hayo kwa wakulima wadogo ambapo kwa kipindi October 2021 hadi hivi  sasa imeweza kuuza nje ya nchi tani 500 ya mazao yanayozalishwa wakulima wadogo.

Akitoa taarifa kuhusiana sekta hiyo katika kikao cha Baraza la wafanyabiashara mkoa wa Arusha  Meneja wa miradi na maendeleo kutoka asasi hiyo Antony Chamanga alisema kuwa asasi hiyo yenye jumla ya wanachama wakulima 15,0000 wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali na katika mnyororo wa thamani wameweza kuleta minyororo ya thamani mipya(mazao mapya) ambayo wanazalishwa kwaajili ya soko la nje.

Alisema kuwa mkoa wa Arusha Kuna uwekezaji mbalimbali wa mazao ya horticulture uliofanyika ambapo makampuni yamewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 133 huku makampuni mengine yanayojishusha na uingizaji(input) yakiwa yamewekeza zaidia ya Bilioni 50 huku wakulima wadogo wakiwa wamewekeza kwenye masuala ya umwagiliaji  na mengineyo kwa kiasi kisichopungua Bilioni 40.

“ Mkoa wa Arusha kwa jiografia  imezungukwa na mikoa mbalimbali ambayo hailimi kwa kiasi kikubwa mazao ya horticulture kwahiyo fursa ya masoko kwa mkoa wetu ni kubwa mnoo, masoko kwa maana ya hapa ndani ya mkoa  lakini pia kuna soko kubwa Nairobi, Mombasa, Dodoma na Dar es salaam,” Alisema.

 “Mwaka jana kwa takwimu ya kitaifa nchi yetu imeweza kupeleka Kenya tani 37240 na kiasi hiki kikubwa kimepitia kwenye mpaka wa Namanga kwa maana hiyotunaona kuwa Arusha ni sehemu muhimu katika kuzalisha lakini pia kupitisha mazao ya horticulture na kwa kupitia haya mkoa wetu utaweza kunufaika,” Alieleza  Chamanga.

Alifafanua kuwa kuna mazao ambayo ni yakipekee ambayo kwa Africa mashariki yanazalishwa Arusha tuu kwaajili ya matumizi ya ndani lakini pia wanapeleka nje ambapo mwaka juzi walifungua Commonwealth facility ambayo wadau mbalimbali wanaweza wakafungasha mazao yao ambayo wanaweza kupeleka hasa hasa katika masoko ya nje ambayo inatoa fursa hata kwa wale wanaoanza biashara ya mazao ya horticulture kwa kuingia katika biashara hiyo bila kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha.

Sambamba na hayo pia alisema kuwa TAHA unafanya kazi na wakulima wengi wa mkoa wa Arusha ambapo wameanzisha kongani kulingana na eneo linaweza kuzalisha kwa wingi zao gani ambapo Wana kongani za Karoti, Vitunguu, Nyanya, Parachichi nakuendea 

Aidha alisema kuwa kama mkoa Kuna masuala mbalimbali ambayo wanatakiwa kuyafanyia kazi ikiwemo kuwa na makampuni mengi zaidi ambayo yatafanya kazi na wakulima wadogo ambayo itaweza kuongeza wigo wa masoko  lakini pia suala la mabadiliko ya tabia ya nchi mbalo linaloathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji kutokana na kupungua kwa mvua pamoja na uwepo wa magonjwa ya mimea ikiwa ni pamoja na bei za kusafirisha nje mazao, pamoja na serikali kuharakisha katika jambo linaloendelea katika mashamba ya maua ambayo yalifungwa awali.

About the author

mzalendoeditor