Featured Kitaifa

MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma.  Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMSEMI, Angellah Kairuki  na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary, Semyamule.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassim Majaliwa ,akisisitiza kwa washiriki wakati akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki,akizungumza wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma baada ya kufunga  Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18, 2023. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kisa Kasongwa baada ya kufunga  Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18, 2023. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Wilaya baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoamalizika leo MACHI 18,2023 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Adolf Ndunguru. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023   jijini Dodoma. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Na.Alex Sonna-DODOMA

 

WAZIRI  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutatua migogoro iliyopo kwenye maeneo yao na sio kusubiri kiongozi mwingine aje asikilize malalamiko ya wananchi.

Hayo ameyasema leo Machi 18, 2023 jijini Dodoma wakati akifunga Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyofanyika kwa siku sita.

Amesema kuwa wakuu wa wilaya mnatakiwa kwenda kutatua mgogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili muweze kuwasaidia wananchi katika masuala hayo.

“Wewe upo hapo unataka Waziri aje aanze kusikiliza kero za mipaka ya vijiji  wakati wewe upo,viongozi wa dini wapo,viongozi wa kimila wapo,nenda kasimamie uimarishaji wa mahusiano ya wadau ndani na nje ya nchi,”amesema Mhe.Majaliwa

Aidha amewataka kusimamai  utoaji wa huduma za jamii katika maeneo  yao kuhakikisheni suala la elimu limetengamaa wanafunzi wanaenda shuleni na madarasa yapo ya kutosha.

 “Miundombinu iimarishwe kupitia mapato ya ndani, huduma za afya zitolewe pamoja na kutatua migogoro ya watumishi wa umma na wanachi”amesema 

Hata hivyo  amewataka kusimamia ajenda za kitaifa ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ili wananchi wapate huduma inayostahili bila ya kudaiwa au kutoa chochote.

Amesema wananchi wanalalamika uwepo wa rushwa unaopelekea haki kutotendeka hivyo ni wajibu wao kufuatilia na kuziba mianya yote ya rushwa katika maeneo yao.
“Mkuu wa wilaya ni wajibu wako kuhakikisha huduma zote wananchi wanazipata bila ya kudaiwa fedha za ziada,watu wasitengeneze mianya ya kudai rushwa,mtu anakuja ana shida anazungushwa nenda rudi kesho alimradi tu atoe chochote,”amefafanua

Akizungumzia ruhusa ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa,Waziri Mkuu amewataka kutumia miongozo iliyopo iliyoainisha juu ya ufanyikaji wa mikutano hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki , amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna bora ya uongozi,kusimamia rasilimali za fedha na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi wa maamuzi.

“Katika mafunzo haya mada 17 zimewasilishwa,ni imani yetu kuwa baada ya mafunzo haya watakuwa wameiva na hata utendaji kazi wao utabadilika,rai yangu kwenu wakuu wa wilaya mkatekeleze yale mliyofundishwa ili kuharakisha utekelezaji wa shughuli za serikali na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),” 

“Tunaamini mkirudi katika maeneo yenu ya kazi mtatekeleza yale yote mliyoelekezwa kwa kushirikiana na viongozi wenzenu, watumishi wa umma na wadau na kuepuka migogoro ya kiutendaji katika maeneo yenu ya kazi” ameeleza Mhe.Kairuki

About the author

mzalendoeditor