Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa zoezi la kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Mkoa wa Dodoma.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TANAPA Dkt.Noelia Myonga,akizungumza wakati akitangaza mafanikio ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita Mkoa wa Dodoma.
Na Erick Mungele-DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wameendelea kuhamasisha Utalii ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza watalii kutoka 1,500,000 hadi kufikia watalii 5,000,000 na kuongeza ukusanyaji wa mapato yatokanayo na utalii.
Hayo ameyasema wakati wa zoezi la kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa taasisi zilizopo Mkoani humo katika miaka miwili ya awamu ya sita ambapo wanajivunia mafanikio ya TANAPA katika Mkoa wa Dodoma kutangaza utalii wa ndani.
Amesema Mkoa wa Dodoma unaendelea kunufaika na sekta hiyo kupitia utalii wa aina mbalimbali kama historia na mali za kale eneo lililotumiwa na wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa bara la Afrika lililopo Kongwa mjini, utalii wa zabibu na mazao yake kama mvinyo pia utalii wa kutembelea mapori ya akiba ya Mkungunero na Swagaswaga.
“Mkoa wetu wa Dodoma kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania limeendelea kuhamasisha Utalii ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii ili kuongeza watalii kutoka 1,500,000 hadi kufikia watalii 5,000,000 na kuongeza ukusanyaji wa mapato yatokanayo na utalii,”amesema senyamule.
Hata hivyo Serikali imeendelea kuboresha Miundombinu na Huduma za Utalii katika maeneo ya Hifadhi za Taifa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kufungua miundo mbinu ya Barabara, Viwanja vya ndege na kuboresha malazi ya watalii na Mkoa wa Dodoma ikijumuishwa.
Kwa upande wake,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TANAPA Dkt.Noelia Myonga amempongeza Raisi wa Jamuhuri wa muungano watanzania kwa kuzindua filamu ya royal tour maana Mafanikio makubwa yameonekana baada ya kuzindua Filamu hiyo.
Amesema Mwaka 2021/2022 hali ya utalii ilianza kuimarika ukilinganisha na mwaka wa fedha wa 2020/2021, ambapo jumla ya watalii 1,053,701 walitembelea Hifadhi za Taifa Tanzania ikiwa ni aongezeko la Watalii 551,759 ukilinganisha na mwaka 2020/2021.
“tunapongeza Raisi wa jamuhuri wa muungano watanzania kwa kuzindua filamu ya royal tour maana Mafanikio makubwa yameonekana baada ya kuzindua Filamu amabapo Mwaka 2021/2022 hali ya utalii ilianza kuimarika ukilinganisha na mwaka wa fedha wa 2020/2021, ambapo jumla ya watalii 1,053,701 walitembelea Hifadhi za Taifa Tanzania ikiwa ni aongezeko la Watalii 551,759 ukilinganisha na mwaka 2020/2021,”amesema Dkt.Myonga.
Pia amesema wamejiweka malengo Kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi kwa kutumia mitandao ya kijamii, kama vile Twitter, WhatsApp, Instagram, YouTube, Facebook na Tiktok na Kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa, Makongamano na Road Shows Pamoja pai Kushirikiana na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi.
Menejimenti ya TANAPA imepongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha mafanikio mengi kwa kipindi kifupi, hivyo kufanya shughuli za Shirika kuendelea vizuri na kwa ufanisi.