Featured Kitaifa

RC DODOMA AZINDUA BARAZA LA BIASHARA MKOA,ATOA MAAGIZO KWA WAJUMBE

Written by mzalendoeditor
MKUU  wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lililozinduliwa Februari 25,2023 jijini Dodoma. 
KATIBU Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akielezea mpango mkakati wa Baraza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lililozinduliwa Februari 25,2023 jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Biashara la Mkoa huo, Khamis Fungameza,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lililozinduliwa Februari 25,2023 jijini Dodoma. 
Afisa Biashara Mkuu Kitengo cha Maboresho ya Mazingira ya Biashara kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw.Julius Mwambeso,akichangia mada wakati wa  uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lililozinduliwa Februari 25,2023 jijini Dodoma. 

SEHEMU  ya wajumbe wa Baraza hilo wakifatilia mada mbalimbali wakati wa  uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lililozinduliwa Februari 25,2023 jijini Dodoma. 

Na.Alex Sonna-DODOMA 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,amewataka wajumbe wa Baraza la Biashara la Mkoa  ngazi ya wilaya kwenda kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo yatavutia wageni kuwekeza katika halmashauri zao.

Hayo ameyasema Februari 24,2023 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara Mkoa huo lenye mpango mkakati wa kuifanya Dodoma kwa kitivo cha Biashara na Uwekezaji nchini.

RC Senyamule amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita imeendelea  kuleta wawekezaji kutoka nje na wanaingia kwa wingi nchini hivyo lazima mkoa na halmashauri zake zikatenge maeneo ambayo yatakuwa rafiki kwa wawekezaji pindi watakapokuja kuwekeza.

”Mkoa wa Dodoma tunataka tuwe na mchango Mkubwa kwenye Biashara hivyo ni matarajio yangu Baraza la Mkoa litakua bora na lenye utashi wa kipekee kwenye makao makuu ya nchi

”Hivyo nawaomba  wajumbe wa Baraza hilo ngazi ya wilaya kwenda kufanya vikao vya mabaraza pamoja na wale wa Halmashauri, Wakurugenzi nao wakafanye hivyo,pia muende mkatenge maeneo ya uwekezaji ambayo yatavutia wageni watakapohitaji kwenda kuwekeza kwenye Halmashauri zenu. ”amesema RC Senyamule

Kwa upande wake  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga,amesema kuwa lengo la Baraza hilo ni kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha Biashara nchini .

”Malengo madogo yakiwa ni kuwa na mpango mkakati wa kufanya kazi ndani ya miaka mitatu, kutangaza shughuli za Biashara na fursa za uwekezaji kupitia vyombo vya biashara, kuongeza idadi ya uwekezaji unaofanyika Dodoma, maeneo ya uwekezaji yaliyotwaliwa yapimwe ili yaboreshwe, mabaraza ya Wilaya yaboreshwe pamoja na kuongeza wafanyabiashara” amesema Dkt. Mganga

About the author

mzalendoeditor