Featured Kitaifa

TAWA YATETA NA VIONGOZI WANAOLIZUNGUKA PORI LA AKIBA KILOMBERO

Written by mzalendoeditor

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekutana na kufanya kikao na viongozi mbalimbali wanaolizunguka Pori la Akiba Kilombero tarehe 23 Februari, 2023, Mkoani Morogoro.

Kikao hiko kililenga kujadili shughuli za uhifadhi wa Pori la Akiba Kilombero na kupanga mikakati ya ushirikiano katika utekelezaji wa Tangazo la Serikali Na. 64 lililoianzisha Pori la Akiba Kilombero.

Tangazo hilo lilitolewa 17 Februari, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kilijumuisha, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe. Sebastian Waryuba, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mhe. Julius Ningu na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Dunstan Kyobya.

Wengine waliohudhuria kikao hiko ni pamoja Wakurugenzi wa Wilaya za Mlimba na Ulanga na Makatibu Tawala wa Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Kilombero.

About the author

mzalendoeditor