Featured Kitaifa

MKURUGENZI WA MPIMBWE AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KWA KUWA MSTARI WA MBELE UHAMASISHAJI CHANJO YA SURUA

Written by mzalendoeditor

Na.Elimu ya Afya Kwa Umma.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi Catherine Mashalla ameiopongeza Wizara ya Afya,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya Kwa Umma Kwa kuweka Kambi katika Halmashauri hiyo Kwa ajili ya kuelimisha Kuhusu umuhimu wa chanjo ya Ugonjwa wa Surua.

Akizungumza ofisini kwake mapema leo Februari 22,2023 baada ya kutembelewa na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Bi.Mashalla amesema hatua hiyo ya timu ya Wizara kuweka Kambi itasaidia kuongeza nguvu katika utoaji wa Elimu juu ya ungonjwa WA Surua unaowakumba watoto.

Hivyo amesema wao kama Halmashauri Kwa kushirikiana na timu za uhamasishaji watashirikiana vyema na Wizara.

“Naishukuru sana Wizara ya Afya Kwa kulibeba hili katika kuhakikisha tunashirikiana Kwa pamoja Elimu na Uhamasishaji Kwa jamii,sisi kama wenyeji tunaungana nanyi hasa kwa kutumia magari ya Matangazo”amesema.

Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Dkt.Martin Laay ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya Kutuma Wataalamu wa Wa Elimu ya Afya kwa Umma na ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia kazi ya kuelimisha na kuongeza kuwa ni muhimu zaidi Timu hiyo ya Wataalamu kutoka Wizara ya Afya , Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kuendelea kuwepo katika maeneo hayo ili kuendelea kutoa Elimu na kuwajengea uwezo zaidi katika kujifunza namna ya kutumia mbinu mbalimbali katika kuelimisha Jamii pindi Magonjwa yanapotokea .

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya,Idara ya Kinga, Elimu ya Afya Kwa Umma Simon Nzilibili amesema wao kama Wizara watahakikisha Elimu inatolewa zaidi Kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo wafugaji,watu wenye ushawishi Ili kuondoa dhana potofu kuwa mtoto mwenye Surua amelogwa.

“Tuna wajibu wa kuhakikisha tunashirikiana zaidi katika utoaji wa Elimu,tutatumia magari ya Matangazo na mbinu nyingine za uhamasishaji”amesema Nzilibili.

Ikumbukwe kuwa Ugonjwa wa Surua husababishwa na Virusi na huambukiza rika lolote lakini huathiri zaidi watoto na moja ya dalili zake ni kukohoa,koo kuuma,madoa ya rangi ya Kijivu na nyeupe sehemu ya ndani ya mashavu,upele mwekundu na macho kuwa mekundu.

Hivyo,baada ya kuripotiwa visa vya Ugonjwa wa Surua katika Mkoa wa Katavi Wizara ya Afya imeshatuma timu ya wataalam Kwa ajili Elimu ya uhamasishaji Chanjo ya Surua huku Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akitarajia kuwasili Februari 23.2023 na siku ya Ijumaa Februari 24,2023 atafanya Mkutano na wananchi katika eneo la Majimoto Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi.

About the author

mzalendoeditor