Featured Michezo

YANGA YAONYESHA UMWAMBA NYUMBANI,YAZOA MAMILIONI YA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor
Na.Alex Sonna-MZALENDO BLOG
WAWAKILISHI katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga wamevuna shilingi  15 milioni za ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kununua kila bao moja Sh5 milioni baada ya kuichapa mabao 3-1 TP Mazembe mchezo wa Kundi D uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na  wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo la usajili Kenedy Musonda dakika ya 7 na Mudathir Yahya dakika 11. 
Kipindi cha Pili Mazembe walipata bao kupitia kwa Alex Ngonga  kwa Mpira wa Faulo ulienda moja kwa moja dakika ya 80 na katika dakika ya 90 +2 Tuisila Kisinda alipingilia msumari wa tatu.
Kwa Matokeo hayo Yanga wapata pointi 3 sawa na Mazembe wakiwa na tofauti ya uwiano ya mabao ya kufungwa na kufunga na kushika nafasi ya tatu huku Mazembe akishika nafasi ya pili ,nafasi ya kwanza inashikwa na US Monastir wenye pointi 4 baada ya kupata sare dhidi ya AS Real Bamko ambao wanshika mkia wakiwa pointi 1 

About the author

mzalendoeditor