Featured Kitaifa

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU VITABU 16

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza uamuzi wa kufuta vitabu 16  leo Februari 13,2023 jijini Dodoma na

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, imepiga marufuku vitabu 16 ambavyo maudhui yake yanakwenda kinyume na mila, desturi na tamaduni za kitanzania.

Akitangaza uamuzi huo leo Februari 13,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, amesema shule yeyote itakayobainika kuwa na vitabu hivyo hatua kali zitachukuliwa ikiwamo kufutiwa a usajili wa shule husika.

Prof.Mkenda,amesema kuwa  vitabu hivyo havipaswi kutumika shuleni na taasisi za elimu kwa kuwa vinakinzana na mila, desturi na utamaduni wa mtanzania.

“Vitabu hivi vinahatarisha malezi ya watoto na vijana wetu, vitabu vinanavyopigwa marufuku ambavyo orodha imetolewa ni pamoja na diary of a wimpy kid, diary of a wimpy kid-Rodrick rules, diary of a wimpy kid-the last straw, diary of a wimpy kid-dog days, diary of a wimpy kid-the ugly truth, diary of wimpy kid-cabin fever, diary of a wimpy kid-the third wheel, diary of a wimpy kid-hard luck,”amesema Prof.Mkenda

Waziri Mkenda amevitaja vingine kuwa ni diary of a wimpy kid-the long haul, diary of wimpy kid-old school, diary of a wimpy kid-double down, diary of wimpy kid-the gateway, diary of wimpy kid-diper overlode, Is for tansgender(you know best who you are), Is for LGBTQIA(find the words that make you you) na sex education a guide to life.

Prof.Mkenda amesema vitabu hivyo vikikutwa shuleni watakuwa wamevunja sheria na hatua kali zitachukuliwa huku wazazi wakihimizwa kukagua mabegi ya shule ya watoto wao ili kuhakikisha havitumiki nyumbani.

“Hii ni orodha ya kwanza ya vitabu baada ya kufanyika ukaguzi na kuhakikiwa, ukaguzi bado unaendelea tunahimiza wazazi, walimu, wanafunzi na mtu yeyote atakayegundua kitabu ambacho kinakinzana na maudhui apige simu kwenye kituo cha huduma kwa mteja kwa namba 02621602270 au 0737 962965,”amesema

About the author

mzalendoeditor