WAWAKILISHI Pekee Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Timu ya Yanga SC imeanza vibaya katika Michuano hiyo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wenyeji Us Monastir Mchezo uliopigwa katika uwanja wa Olympic Rades-Tunis nchini Tunisia.
Mabao ya wenyeji yamefungwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 10 likifungwa na Mohamed Saghroui kwa kichwa mpira wa faulo na dakika ya 15 likifungwa na Mshambuliaji wa Mali Boubacar Traore.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na hakuna timu yoyote ambayo iliweza kupata bao katika kipindi hicho
Matokeo Mengine ya Kundi D TP Mazembe waichapa mabao 3-1 As Real Bamako kutoka nchini Mali,Sasa Mazembe wanaongoza kundi hilo nafasi ya pili Us Monastir,As Real Bamako na Yanga zote hazina pointi.
Yanga SC watashuka uwanjani mnamo Februari 19 kumenyana na TP Mazembe mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.