Featured Kitaifa

WADAU SEKTA YA UMMA NA BINAFSI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANASAYANSI WANAWAKE NA WASICHANA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Prof.Maulilio Kipanyula,,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (hayupo pichani),wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi  Naibu  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (hayupo pichani)  mara baada ya kuhutubia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuhutubia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

……………………………………

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,amewataka wadau wa sekta ya umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za wanasayansi wanawake na wasichana kuimarisha mchango wa utafiti na ubunifu wenye tija kwa ustawi wa uchumi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 11,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu.

Kipanga amesema kuwa maadhimisho hayo yana umuhimu wa kuhamasisha wanawake na wasichana kuwa wanasayansi ili kuchochea maendeleo ya nchi.

“Ubunifu wa wanawake na wasichana ni unahitajika na unachangia kikamilifu katika maendeleo hayo, tunafarijika sana kuona watanzania hasa wanawake na wasichana wanazalisha bunifu nzuri,”amesema Kipanga

Aidha amesema kuwa serikali inaendelea kuwekeza na kuwezesha kwenye miundombinu ya rasilimali watu itakayowezesha kufanyika utafiti wa kisayansi wa kuzalisha bunifu zinazojibu kero za watanzania ili kukuza sekta ya viwanda na za kipaumbele ifikapo 2025.

Hata hivyo wito kwa wazazi na jamii kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi na ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo,amesema kuwa bunge linatambua umuhimu wa kumkomboa mtoto wa kike katika kumpatia elimu hasa elimu ya sayansi, hesabu na ubunifu.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 24 pekee ya wanafunzi wa kike waliopo vyuoni wanasoma masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.

About the author

mzalendoeditor