WAWAKILISHI katika Michuano ya klabu Bingwa Afrika Timu ya Simba SC imeanza vibaya baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Horoya AC mchezo uliopigwa nchini Guinea.
Wenyeji walipata bao dakika ya 18 likifungwa na Pape N’diaye kwa kichwa akimalizia mpira wa Kona mnamo dakika ya 80 Horoya walikosa Penalti iliyopanguliwa na Aishi Manula.
Kwa ushindi huo Horoya wameshika nafasi ya pili wakiwa na Pointi tatu sawa na Casablanca wakiongoza kwa wingi wa mabao baada ya kuichapa Vipers SC mabao 5-0.Simba SC akishika nafasi ya tatu akiwa hana Pointi huku Vipers wakishika Mkia.