Naibu Waziri wa Maendeleo Ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Mwanaidi Ali Khamis akifungua Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati yanayofanyika Tarehe 09-10/02/2023, Mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Bi Rennie Gondwe akizungumza katika Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati Yanayofanyika Tarehe 09-10/2023 ,Mjini Morogoro.
Afisa MaedeleoyaJamii wa Mkoa wa Morogoro Tumaini Wapalila akizungumza katika Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati yanoyofanyika Tarehe 09-10/02/2023 ,Mjini Morogoro.
Kamishna Msaidizi wa Mkoa Wa Morogoro Bi Zarau Mpangule akizungumza katika Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati yaliyofanyika Tarehe 09/02/2023 Mjini Morogoro.
Mwezeshaji wa Masuala ya Madawati ya Jinsia Kutoka Ofisi ya Rais -Utumishi Ndugu Staricko Meshack akiongoza Mada katika Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati Yanayofanyika Tarehe 09-10/02/2023 Mjini Morogoro.
Baadhi ya Washiriki katika Mafunzo ya uanzishwaji,Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu YaJuu Na Elimu Kati yaliyofanyika Tarehe 09/02/2023 Mjini Morogoro.
Picha zote na kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM.
…….
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Mwanaidi Ali Khamis amesema Serikali imedhamilia kuondoa Ukatili wa Kijinsia Nchini Kwa kuja na Mpango kazi unaotekelezeka ikiwemo Uanzishaji wa Madawati ya Kijinsia Kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati.
Amesema hayo alipokua akifungua Mafunzo ya uanzishwaji, Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Dawati la Jinsia Kwa Wakuu wa Vyuo na Waratibu Wa Madawati kwa Taasisi Za Elimu ya Juu na Elimu kati Mafunzo yatayofanyika kwa Siku mbili mkoani Morogoro kuanzia Februari 09, 2023
“Nawapongeza Wale wote ambao wameshafungua Madawati lakini pia Nawapongeza wale ambao hawajafungua bado na wamefika hapa leo ili kujifunza namna ya kufungua na Kuendesha Madawati hayo ili kukabiliana na Ukatili unaondelea Nchini” Alisema Mwanaidi Ali Khamis.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema uanzishwaji wa Madawati ya Jinsia Kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo Vya Kati ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2000 ambayo ilianza kutekelezwa Mwaka 2005.
“Tunazindua Madawati haya na Tutaunda Tume itakayofatilia Utendaji kazi wa Madawati haya kwa sababu Vitendo vya ukatili wa Kijinsia viko juu na Watoto wa kike wamekuwa Wahanga wakubwa”
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Rennie Gondwe, amesema Mafunzo hayo kwa wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati ni Muendelezo wa Jitihada za Serikali kupambana na Ukatili wa kijinsia
“Hii ni awamu ya pili,Tulianza Mafunzo haya kwa Wakuu wa Vyuo vilivyopo Mkoa wa Dar es salaam, na katika awamu hii Mafunzo yanafanyika kwa Wakuu wa Vyuo vilivyopo Pwani,Tanga na Morogoro .Tutaendelea kufanya Mafunzo haya na kuhakikisha Mikoa yote inafikiwa” amesema Gondwe.
Naye, Profesa Musa Assad kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro(Morogoro Muslim University) amesema Vitendo vya ukatili uliokithiri hasa kwenye vyuo vinasababishwa na mmonyoko wa Maadili.
“Chanzo kikubwa cha Kuongezeka kwa Matendo haya ya Ukatili ni mmonyoko wa maadili ulio kithiri ndani ya Jamii ,Watu hawana hofu ya Mungu na Vijana hawana nidhamu hivyo ili kurekebisha hili inabidi tupambane kurudisha nidhamu kwa Wanajamii”alisema Profesa Assad.