Featured Kitaifa

MKURUGENZI MKUU EWURA DKT.ANDILILE AKABIDHIWA OFISI

Written by mzalendoeditor

 

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile ( kulia) akipokea kitabu cha Sheria mbalimbali za kiudhibiti kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu. Mha. Modestus Lumato, wakati akikabidhiwa ofisi leo Februari 8,2023  jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile,akisalimiana na baadhi wafanyakazi katika ofisi za EWURA Makao Makuu, Dodoma leo Februari 8,2023.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa EWURA, katika ofisi za EWURA, mara baada ya kukabidhiwa Ofisi leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.
……………………….
Mkurugenzi Mkuu mpya wa EWURA, Dkt. James Andilile, leo tarehe 8/02/2023 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Mha. Modestus Lumato.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Andilile alisema: “Tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza majukumu ambayo Serikali imetuamini, ili tuendelee kuwatumikia Watanzania, kwani huduma za nishati na maji zinagusa Wananchi moja kwa moja”
Dkt. Andilile, ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  Tar. 3 Feb, 2023.

About the author

mzalendoeditor