Featured Michezo

ARSENAL HAISHIKIKI YAICHAPA MANCHESTER UNITED

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Arsenal FC imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kutoka nyuma na kuichapa  mabao 3-2 Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah mawili, dakika ya 24 na 90 na Bukayo Saka dakika ya 53, wakati ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 17 na Lisandro Martínez dakika ya 59.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 19 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City waliocheza mechi 20 wakiwa na Pointi 45 wakati Manchester United inabaki na pointi zake 39 za mechi 20 nafasi ya nne.

About the author

mzalendoeditor