Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AUPONGEZA MKOA WA DODOMA KWA UWEKEZAJI

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa kutangaza mafaniko ya serikali ya awamu sita kwa kipindi cha miaka miwili ya kuwa madarakani ulioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango hafla iliyofanyika leo Januari 20,2023 jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa Mkutano wa kutangaza mafaniko ya serikali ya awamu sita kwa kipindi cha miaka miwili ya kuwa madarakani ulioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 20,2023 jijini Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akizungumza wakati wa Mkutano wa kutangaza mafaniko ya serikali ya awamu sita kwa kipindi cha miaka miwili ya kuwa madarakani ulioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika leo Januari 20,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki, wakati akifungua Mkutano wa kutangaza mafaniko ya serikali ya awamu sita kwa kipindi cha miaka miwili ya kuwa madarakani ulioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango hafla iliyofanyika leo Januari 20,2023 jijini Dodoma.

………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Isdori Mpango,ameupongeza Mkoa wa Dodoma kwa jitihada kubwa za kuhakikisha inatoa kipaumbele katika eneo la uwekezaji.
Hayo yamesemwa leo Januari 20, 2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Angellah Kairuki,wakati akisoma hotuba kwa niaba ya  Makamu wa Rais katika hafla ya kutangaza mafaniko ya serikali ya awamu sita kwa kipindi cha miaka miwili ya kuwa madarakani ulioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Waziri Kairuki amewapongeza  kwa kuwekeza katika soko la machinga lililojengwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Serikali ,hii inadhihirisha jinsi ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan inavyojali vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaotafuta riziki yao kwa njia za halali.
“Nichukue fursa hii pia kumpongeza Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi hichi cha miaka miwili toka agie madarakani uchumi wetu umendelea kuimarika siku hadi siku”amesema Waziri Kairuki

Aidha amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo kwa kuhakikisha kuwa kila eneo la ardhi amablo linafa kwa kilimo linalimwa ili kuongeza uzalishaji na kuwa na uhakika wa chakula.

Waziri Kairuki amewataka Machinga nchini kuhakikisha kuwa wanahamia bila usumbufu katika maeneo ambayo serikali ya awamu sita imewekeza fedha nyingi kuwajengea.

“Na niwaombe wamachinga na wafanyabiashara ndogo ndogo kuitika wito wa Serikali unaowataka kuhamia katika maeneo yaliyoboreshwa bila usumbufu wowote. Ninaamini hata wao wanapenda kuwahudumia wateja wao katika mazingira bora zaidi,”amefafanua.

Amesema, kuwaweka vijana wajasiriamali wadogo pamoja, kumefanya Jiji la Dodoma lianze kuonekana safi na lenye mazingira bora.
“Nizitake halmashauri zote nchini kutenga na kuyaendeleza maeneo maalumu kwa ajili ya wamachinga na wafanyabiashara wadogo wadogo.
Hata hivyo Waziri Kairuki amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja  kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma.
”Yapo maeneo yaliyotayarishwa kwa ajili ya uwekezaji kwenye viwanda vya aina zote, biashara ikiwemo shopping malls, supermarkets, maduka madogomadogo, viwanja vya michezo ikiwemo vya golf course,hoteli hususani hoteli za hadhi ya nyota tatu na maeneo maalum kiuchumi.”amesema

Awali Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kiasi kingi cha fedha kutekeleza miradai mbalimbali ya maendeleo.

”Mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa mkoa wa Dodoma katika kipindi cha miaka miwili ni pamoja na kuongezeka kwa bajeti ya sekretarieti ya mkoa na halamashauri imeongezeka kutoka Sh.314,945,766,645 mwaka 2020/21 hadi Sh.372,065,282,000 mwaka 2022/23.”amesema Senyamule

Mhe.Senyamule amesema kuwa ongezeko hilo limesadia kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi katika mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Spika Mstaafu Mhe.Job Ndugai amewataka Watanzania kutoitegemea serikali kwa kila kitu bali kila mmoja atimize wajibu wake katika kushiriki shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ili kujikwamua kichumi.

About the author

mzalendoeditor