Featured Michezo

SIMBA SC YAICHAPA MBEYA CITY

Written by mzalendoeditor

 

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa kuichapa Mbeya  City kwa mabao 3-2, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Bejamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Saidi Ntibazonkiza dakika 11, aliefunga bao zuri na kuhamsha shangwe za mashabiki waliongia kwenye uwanja huo kushuhudia mchezo  huo ambao ulikuwa wa aina yake.

Ntibazonkiza ameendelea kuuwasha moto ndani ya uzi  wa msimbazi baada ya kufanikiwa kupachika bao la pili dakika 49 ambalo likafanya afikishe mabao tisa kwenye ligi hiyo.

Bao la tatu Simba Sc limefungwa na Pape Sakho dakika ya 56 ya mchezo,  huku mabao ya  Mbeya City yakifungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 13  na bao la pili likifungwa na Juma Shemvuni dakika ya 78 na mechi kuisha Simba Sc kuondoka na ushindi wa mabao 3-2.

Kwa ushindi huo Simba SC imefika Pointi 47 ikibaki nafasi ya pili huku Yanga bado anaongoza Ligi akiwa na Pointi wote wakicheza mechi 20.

About the author

mzalendoeditor