ARSENAL wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachapa wapinzani wao wa London Derby mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Hugo Lloris aliyejifunga dakika ya 14 na Martin Odegaard dakika ya 36 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 47 na kutanua uongozi wao kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18.
Kwa upande wao, Tottenham Hotspur baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 33 za mechi 19 nafasi ya tano.