Featured Kitaifa

CHANZO CHA MAJI CHAMLAZIMU WAZIRI AWESO KUTUMIA BODABODA

Written by mzalendoeditor

Waziri Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa Mkoani Morogoro Katika Ziara yake amefika katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambapo ametembelea na kukagua mradi wa maji Morong’anya unaogharimu kiasi Cha Tshs 23,186,021,991 ambapo pindi utakapo kamilika utahudumia wananchi zaidi 52,000 kwenye vijiji 19 vilivyopo katika kata 7 za Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Pamoja na changamoto za Barabara ya kuelekea eneo la chanzo kilipo kutofikika kwa gari Mhe. Aweso akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo Hilo Hamisi Tale Tale pamoja na viongozi wengine wa chama walilazimika kutumia usafiri wa pikipiki ambapo aliweza kufika kwenye chanzo na kufurahishwa na Maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo.

Aidha Mhe. Waziri ameweza kushiriki zoezi la kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha mto Mbezi utakaotumika kama chanzo cha maji kwa mradi huu mkubwa na wakihistoria katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki na Wilaya ya Morogoro kwa ujumla lakini pia ameweza kushiriki kazi ya kuunganisha mabomba na kuyalaza ikiwa ni moja ya juhudi za utekelezaji wa Mradi huu.

About the author

mzalendoeditor