Featured Kitaifa

VIJANA WAASWA KUTAMBUA FURSA NA KUZITUMIA KATIKA MAENEO YAO

Written by mzalendoeditor
Baadhi ya Watawa kutoka katika Majimbo mbalimbali Katoliki Tanzania wakiwa katika Semina kwenye Kongamano la 14 la TMCS Kitaifa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Marian -Bagamoyo Jimbo Katoliki la Morogoro (Picha na Ndahani Lugunya)
………………………………….
Na Ndahani Lugunya,Bagamoyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment Dkt Fredi Msemwa amesema kwamba,kitendo cha kijana chakuzaliwa Tanzania  ni mtaji wa kwanza katika kuibua na kutumia fursa za kiuchumi,hivyo vijana wanapaswa kujivunia utanzania  wao ili kutumia rasilimali za nchi kujiinuakiuchumi.
Dkt Msemwa amesema hayo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 14 la Umoja  wa Wanafunzi Wakatoliki wanasoma Vyuona Vyuo Vikuu Tanzania (TMCS),katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian iliyopo Bagamoyo Mkaoni Pwani.
Amesema kwamba fursa zote zinazokuja mbele ya vijana zinapaswa kuangaliwa kwa umakini,kumbe vijana wanahamasishwa kuwa na uwezo wa kutambua fursa na kuongeza kwamba kutambua fursa peke yake hakutoshi bali watambue fursa na kufanya kwa ubora katika  kuishughulikia fursa hiyo.
Dkt Msemwa amesema kwamba fursa haina maana yoyote kama haitatumiwa  ipasavyo na kwa ukamilifu,kwani kutambua fursa ni jambo moja na kuitumia fursa hiyo ni jambo lingine.
“Fursa ni kitu chochote halali  ambacho kikitumiwa vizuri kinaweza kuleta manufaa.fursa ni lazima iwe ni halali lakini cha pili ni lazima itumikena ndipo itapata sifa ya kuitwa fursa.
Kwa hiyo ninyi katika hatua hii ya ujana fursa mliyonayo kwa sasa nikusoma  fursa ya kujuana na kufahamiana na marafiki  kwani hiyo ni fursa na ni mtaji yaani social capitali kufahamiana na watu ni mtaji tosha kwenu endapo tu mtu huyo nae anajambo ambalo mkiunganisha mnapata kitu ambacho kitawasaidia.
Kwa hiyo kusoma kufahamiana na watu na katika makongamano kama haya,kujua kwamba wapi utakwenda kuomba ushauri kama Viongozi wetu wa kiroho,wazazi,ndugu jamaa na rafiki zetu  zote hizo ni fursa  kwenu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia katika kufikia ndoto zenu,” amesema Dkt Msemwa.
Aidha katika hotuba yake Dkt Msemwa amesema kwamba  Vijana ni lazima wawe na macho ya kutambua fursa,kwani Tanzania  ni miongoni mwa nchi zenye fursa  nyingi za kiuchumi.
Hata hivyo amesisitiza kwamba suala la fursa linakwenda sambamba na suala la ujasiliamali,kumbe vijana watambue mahitaji ya jamii na kubuni bidhaa au mahitaji katika jamii,huku akiongeza  kwamba katika ujasiriamali ni sharti kwamba sualala hasara likachukuliwa kama sehemu ya biashara.
Sanjari na hayo amesema kwamba zipo fursa za kuajiriwa katika sektambalimbali za umma na za binafsi,kumbe  vijna  wanapaswa kuwa na weredi katika kutengeneza mazingira binafasi na ya wasifu kazi ili kuendana na mahitaji ya kazi inayotakiwa. 
DKt Msemwa ameendelea kusema kwamba ni lazima  katika dira ya maisha kijana akatambua kwamba kuna vitu bora kuliko fedha,na miongoni mwa vitu hivyo ni busara,jina zuri,uaminifu.
Amesisitiza kwamba pamoja na bidii kubwa wanazozifanya vijana na hasa walipo katika Vyuo na Vyuo Vikuu,lakini yapo maarifa ya ziada  wanayopaswa kuyazingatiwa  na kupewa uzito mkubwa kutokana na ushindani uliopo katika soko la ajira.
“Sisi tunaojiandaa kuingia katika soko la ajira ni lazima tujijengee uwezo wa kuwana vitu vya ziada,’ amesema Dkt Msemwa. 
Amesema msingi wa wao kuwa vijana ni kutokatishwa tamaa na mtu yoyote na hivyo wajiamini wakijua kwamba wanaweza kufika popote pale wanapohitaji kufika.
Katika hatua nyingine amewata vijana kuwa na uaminifu,bidii na kujisimamia katika mambo yao na kuongeza kuwa,ili kijana aweze kutetea ndoto alizonazo ni lazima aweke msimamo wa kujisimamia.

About the author

mzalendoeditor