Featured Michezo

YANGA HAISHIKIKI NBC LIGI, MAYELE WA MOTO

Written by mzalendoeditor
Na Bolgas Odilo
HIVI ndivyo unavyoweza kusema! Yanga SC ya Moto ,Fiston Mayele wa Moto baada ya kuendelea kichapo kwa wapinzani baada ya kuichapa mabao 3-0  Coastal Unions mchezo wa Ligi Kuu ya NBC  uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 
Yanga walianza kuhesabu mabao dakika ya 28 Mshambuliaji hatari kwa sasa  Fiston Kalala Mayele aliwanyanyua mashabiki.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kunamo dakika ya 47 Fiston Mayele alipachika bao la pili na likiwa bao 13 msimu huu wa Ligi na dakika ya 66 kipenzi cha wanayanga kiungo fundi Feisal Salum (Fei Toto) alipingilia msumari wa tatu.
 
Kwa ushindi huo Yanga wameendelea kukaa kileleni mwa Msimamo wa Ligi kwa kufikisha Pointi 44 na kuiacha Simba kwa tofauti ya Pointi 7 huku Simba wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Mchezo mwingine timu ya Ruvu Shooting imeshindwa kutamba katik  uwanja wake baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.
Ushindi huo wa Yanga 

About the author

mzalendoeditor