Featured Kitaifa

RC MWASA AJIPA JUKUMU KULEA SMAUJATA

Written by mzalendoeditor

  

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa ametangaza kuwa mlezi wa Kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Morogoro kuanzia sasa.

Mhe. Mwasa ametoa kauli hiyo alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kufungua kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati Mkoani humo Desemba 17, 2022

Amesema Kampeni hiyo siyo ya Wizara peke yake bali kwa Mkoa wa Morogoro ni Kampeni ya wananchi wote.

“Nitangaze Rasmi kuanzia leo, Kwa mkoa wa Morogoro mlezi wa SMAUJATA nakuwa mwenyewe, nimejipa hiyo kazi” amesema Mhe. Mwasa.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Gwajima kwa juhudi zake za kupambana vita dhidi ya ukatili, akitaja takwimu za kesi za ukatili Mkoani hapo kwa mwaka 2022 kuwa ni 303 huku kesi zaidi ya 250 zikihusisha ukatili wa kingono.

Akifungua Kongamano hilo, Waziri Gwajima amewaomba Wakuu wa Mikoa wengine kumuunga mkono na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kuwa shujaa namba moja Mkoani hapo, kwani vita ya ukatili itaisha iwapo viongozi wote wataibeba ajenda.

About the author

mzalendoeditor